SIMULIZI…..WHEN
I SAY I LOVE YOU! ( 12 )
MTUNZI…….GIFT KIPAPA
ILIPOISHIA….
“Aah, karibu tena karibu sana!”
Dulla aliongea maneno hayo
mfululizo huku akimsindikiza mpaka alipotoka nje ya saluni hiyo, haikuwa
kawaida yake kuwasindikiza wateja lakini siku hiyo alijikuta anamsindikiza
Rehema.
“Poa basi, karibu sana Ray!”
“Asante , kwaheri!”
Rehema aliitikia huku
akimuangalia Dulla kwa macho malegevu , moyoni mwake alijawa na furaha tupu
alijiona kama vile tayari amekwisha mpata dulla, hakuelewa kwa nini amekuwa na
moyo wa kujiamini kiasi hicho ila moyo wake ulimsitizia kwamba Dulla ni wako
tu, na kujikuta anauamini moyo wake kwa asilimia zote mia kwa mia.
MUENDELEZO WAKE :
Alitembea kwa takribani hatua
kumi na kisha kugeuka nyuma ambapo alikuta Dulla bado amesimama akimuangalia,
alimpungia mkono huku akitabasamu ambapo Dulla nae alitabasamu pia na kuupunga
mkono wake. Kisha Rehema akaendelea na safari yake huku mawazo yake yote yakiwa
yamebaki kwenye saluni hiyo.
Ilikuwa vigumu kwa Dulla kuamini
kile kilichotendeka kwake siku hiyo alihisi labda ilikuwa ndoto au mawazo,
alibaki ameduwaa tu huku akimuangalia Rehema mpaka alipotokomea , kitendo cha
Rehema kumpatia yeye pesa kilivunja rekodi katika moyo wake. Ilikuwa ni ajabu
kwake tena ajabu ambayo hajawahi kuisikia wala kuiona mishani mwake.
“Sijawahi kuona mimi, shori huyu
ni wa aina yake aisee!!”,
Alijisemesha huku bado yupo
katika hali ya kushangaa
“mtoto anaonekana kwo kupo njema,
sasa kwanini mtu mzima nisijishikize!?”,
Dulla alijiuliza swali hilo
kichwani kwake na kujikuta anapata hisia flani moyoni mwake na kujikuta anapata
msukumo wa ajabu juu ya jambo hilo.
“Namfuata nikamweleze sasa
hivi!”,
Dulla aliwaza na dakika hiyo hiyo
alitoka mbio na kusahau hata kufunga mlango wa saluni alielekea kule ambako
Rehema alielekea, alikimbia kwa kasi ili asimkose , Rehema hakuwa mbali sana
kwani haikumchukua muda mrefu akawa amemuona akiwa upande wa pili wa barabara.
Kuna Roli lilikuwa lina pita kwenye barabara hiyo lakini yeye hakulijali
alikatiza haraka kwenye bara bara hiyo .
“Wewe utakufa ,mjinga wewe!!”
Alifoka dereva wa Roli hilo baada
ya kufunga breki ya ghafla
‘kuuuu’
breki hiyo ilisikika ilkuwa
nusura amgonge Dulla,
watu wote waliokuwepo kwenye eneo
hilo waligeuza vichwa vyao ilikuangalia ajali hiyo iliyo nusurika kutokea ,
Rehema pia aligeuka na kuona kwamba mtu aliyenusurika kugongwa na Roli hilo ni
Dulla, moyo ulimpasuka huku akiwa haamini kama kweli Dulla wake ndiye alikuwa
katika hatihati za kugongwa , Dulla mwenyewe hakujali wala kuzingatia maneno
aliyoyasema dereva wa roli yeye aliendelea kukimbia tu.
“Dullaaa!!!”
Rehema aliita kwa sauti
“Ray!!”,
Nae pia aliita huku akizidi kumsogelea.
“Unaenda wapi Dulla!?”,
aliuliza Rehema
“Kwako Ray, nakufuata wewe!”,
aliongea Dulla huku akihema
“Mimi!?”,
aliuliza kwa mshangao
“Ndio wewe Ray kuna kitu nataka
kukueleza!”
“Kitu gani!?”,
“Nakupenda Ray, nimeshindwa
kabisa kuliweka moyoni ,nimeonelea bora nikueleze nakupenda Ray!”.
Dulla aliongea maneno hayo bila
kusita huku akihema sababu ya kukimbia, aliongea kwa urahisi tu bila kujua ni
kwa kiasi gani maneno hayo yalivyokuwa na uzito kwenye moyo wa Rehema , ambaye
mara baada ya kuyasikia maneno hayo mwili wake ulisisimka akajikuta ameyafumba
macho yake kwa hisia huku akihisi moyo wake huko kwenye boxi lenye barafu,
“Ray usinifumbie macho , ninacho kiongea
kinatoka moyoni niamini tafadhari!”,
Dulla alizidi kuongea maneno
yaliyo mfanya rehema azidi kupagawa , aliyafumbua macho yake yaliyo ambatana na
machozi yaliyoanza kububujika kwenye mashavu yake,yalikuwa ni machozi ya
furaha, Rehema hakutegemea kabisa kwamba leo ndio siku ambayo ndoto yake
imekamilika. Furaha aliyokuwa nayo moyoni ilimshinda nguvu bila kujali watu
wakikatiza maeneo hayo wala sare za shule alizozivaa akajikuta amemkumbatia Dulla
huku machozi yakizidi kumtoka na kudondokea mgongoni kwa Dulla.
“Nakupenda dulla zaidi ya unavyo
fikiria nakupenda sana!”
Aliongea maneno hayo huku
akiendelea kulia bila kujua kwamba kilicho mvutia Dulla kwake sio mapenzi bali
ni pesa alizompatia muda mfupi uliopita walipokuwa saluni.
Dulla akajitoa mwilini mwa Rehema
kwani alishaanza kuona aibu kumkumbatia mwanafunzi mbele ya hadhara , sababu
kitendo hicho cha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi kinapigwa vita na
jamii nzima isitoshe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi ni kosa la
jinai hivyo Dulla aliogopwa kukutwa na hatia hiyo kwani alijua angeozea jela.
“Twende saluni basi” aliongea Dulla
“Sawa !”
aliitikia kisha wakaongozana.
Watu wote waliwashangaa kwa
kitendo walicho kifanya huku wengine wakiongea maneno ya kuwa karipia, wao hawakujali
waliendelea na safari yao na kuwaacha watu hao wakibaki na maada.
Wakiwa ndani ya saluni
walizungumza mengi kuhusu penzi lao hilo lililo chipua siku hiyo, Rehema akiwa
mwenye furaha ilioje alimweleza Dulla kila kitu kinacho husu maisha yake ikiwa
ni pamoja na maisha yake ya mapenzi,alifanya hivyo sababu alimuamini kupita
kiasi bila kujua ukweli uliokuwepo kwenye moyo wa Dulla, hakujua kwamba dulla
ni tapeli wa mapenzi, jambo hilo halikuwepo kabisa kichwani mwake masikini ya
mungu.
“”Dulla naukabidhi moyo wangu
mikononi mwako,naomba uutunze kama unavyoitunza mboni ya jicho lako “
“niamini Ray nimeshakueleza
nakupenda!”,
Aliongea Dulla huku nafsi yake
ikimsuta kwamba alichokuwa akikiongea ni uongo mtupu. Aliongea mengi ambayo
yalizidi kumfanya Rehema apagawe kabisa na penzi hilo.
Dulla alikuwa na uzoefu mkubwa katika suala la
mapenzi, alishawahi kuwa na wapenzi lukuki hivyo alijua vema jinsi ya kuweza
kumlaghai msichana yoyote yule, maneno matamu aliyoyatoa kinywani mwake
yaliweza kuwa chambo cha kuweza kumvuta msichana yoyote yule. Rehema hakujua
kwamba maneno yote hayo dulla aliyaongea kwa uzoefu tu.
END OF SEASON ONE
soma msimu wa pili hadi mwisho kwa kununua hadi mwisho au kwa kununua episodi za simulizi hii katika email yako, inbox ya fb au whatsapp kwa sh 100 tu kwa episodi , tsh 1000 kwa episodi kumi , kenye sh ni ksh 10 kwa episodi
No comments:
Post a Comment