BY D.G.LWASYE 'GIFT KIPAPA'
MBEBE MWANAO MTOKE
Mvua kumbwa iliyoambatana
na miungurumo ya radi ilikuwa ikinyesha,
mishale ya saa tatu za za usiku karibu kila
mtu alikuwa amejifungia nyumbani kwake akiutafuta usingizi katika usiku huo
uliokuwa na kibaridi.
"Mamaaaaaaaa!!!!!!"
Ilisikika sauti hiyo ya
mtoto akilia maeneo ya tabata bima jijini dar es salaam.
"Utaniua mume wangu!"
Mwanamke alisikika akilia
kwa uchungu huku sauti za mikanda na mabao zikisikika
"Baba muache
mama!"
Mtoto aliongea huku akilia
kwa uchungu
"Kelele wewe mwana
haramu, mimi sio baba yako!"
Aliongea mwanaume huyo huku
akimwangalia mtoto huyo kwa ghadhabu.
"mume wangu
jamani!!"
Mwanamke aliongea kwa sauti
ya kinyonge
"Pumbavu na wewe kimya
malaya mkumbwa"
Aliongea huku akimgeukia
mwanamke huyo na kisha kumpiga teke zito la tumboni
'Puuuuu'
"Uuuuh"
Mwanamke alilia kwa uchungu
"Nitakuua leo malaya
mkubwa wewe"
aliongea kwa ukali huku akimshushia mvua ya mikanda mwanamke huyo
aliongea kwa ukali huku akimshushia mvua ya mikanda mwanamke huyo
"Nisamehe mume wangu
mwanamke alilalamika lakini badala ya kumhurumia mwanaume huyo ndio kwanza
alizidi kupandwa na hasira, alizidi kumpiga huku akitoa matusi ya nguoni
"Malaya mkumbwa wewe
leo utanikoma!"
"Baba muache mama,
baba naomba babaa"
Mtoto alizidi kuangua kilio
lakini mwanaume huyo
hakujali kauli hiyo ya
mtoto, aliendelea tu kumpiga mwanamke.
Mtoto alishindwa kuvumilia
akaenda kumvaa mwilini baba yake.
"Baba muache mama ,
baba muache, ba....."
Alilia mtoto huyo kwa
uchungu huku akiwa ameishikilia miguu ya baba yake akimsihi aache kumpiga mama
yake.
"Pumbavu mwana haramu
weee!!"
aliongea mwanaume huyo na
kisha kumbutua mtoto huyo kama mpira mpaka kudondokea kwenye meza iliyokuwa
sentimita kadhaa toka pale walipokukuwa
"Mungu wangu!!!!"
aliongea kwa mshituko
mwanamke baada ya kushuudia kitendo hicho cha kinyama alihisi uchungu wote wa
uzazi umejirudia hakuwai kumuona mwanae akiviringika kiasi hicho
"Kelele usiniite tena
mumeo mimi sio mumeo!"
Aliongea kwa ukali na
kuanza tena kumshambulia mwanamke huyo kwa mateke na mangumi.
"Baa,ba...."
Mtoto alitaka kuongea
lakini alitaka kuongea
lakini alishindwa kutokana
na maumivu makali aliyoyapata alipoangukia kwenye meza
"Dany!,Dany!"
Mwanamke aliita huku
akimwangalia mtoto.
"Mama,ma!"
Mtoto nae aliita lakini kwa
taabu na kisha kudondoka chini
"Dany! ,Dany!"
Mwanamke aliita lakini
mtoto hakuitika wala kutikisika pale chini alipodondokea.
"Mmume wangu Dany
ame...."
Alikatishwa na bao zito
lililotua usoni kwake.
"Nimekwishakueleza
mimi sio mume wako"
aliongea mwanaume huyo kwa
ukali
"Lakini mtoto amezimia
Joel!"
Aliongea mwanamke huyo kwa
sauti ya upole
"Kwahiyo kama
amezimia?"
Aliuliza kwa dharau
"Joel kama makosa
nimefanya mimi na sio mtoto"
Mwanamke huyo alizidi
kuongea kwa huruma
"Hilo mimi sijali wewe
na mtoto wako wote sitaki kuwaona"
"Joel jamani!!"
"Joel nini? Beba hicho
kipaka chako utoke nyumbani kwangu sasa hivi"
Aliongea kwa ukali
"Joel jamani!! nisamehe"
"Hakuna cha msamaha
hapa nimeshasema toka!"
Alisisitiza na kuanza
kumsukuma mwanamke huyo ili atoke
"Joel jamani mvua
inanyesha alafu usiku saa hizi"
aliongea mwanamke huyo kwa
huruma
"Usinieleze habari za
mvua mimi nimesema mbebe mwanao mtoke"
alisisitiza mwanaume huyo
kwa ukali, uso wake hakuonyesha hata chembe ya huruma
"Toka usikii?"
alizidi kufoka
"Joel muonee huruma
mtoto mvua hii"
"Mtoto nini mpeleke
kwa baba yake, nimesema mtoke"
alizidi kufoka huku
akimsukumiza, mwanamke huyo alijisogeza mpaka alipo mwanae na kujaribu kumwinua
"Dany, Dany!"
Aaliiita huku akimtikisa
mtoto
"Nimesema toka Edna
nikizidi kusikia hilo jina la kitoto chako unazidi kunichefua, toka
unisikii?"
alifoka Joel huku
akimsukuma Edna.
"Joel jamani kuwa
Binadamu, mvua yote hii kweli tutoke?"
Edna alijaribu kumbembeleza
"ubinadamu! unaujua
ubinadamu wewe? ungekuwa binadamu ungenifanyia yote haya?"
aliongea Joel kwa ukali
"Najua Joel ndio maana
nakuomba msamaha, naomba Joel mvua hii muonee huruma mtoto"
"Mtoto!, mtoto nini si
wako nimesema tokaaaaa"
alizidi kufoka na kuendelea
kumsukumiza, alifungua mlango na kumsukumia nje
"Joel jamani
tuhurumie"
aliongea kwa huruma baada
ya Joel kumsukumiza nje kwenye mvua, yeye na mtoto wake walidondoka chini
kwenye matope
'pwaaaa'
"tokaaaaaaa!"
Joel alifoka na kisha
kuubamiza mlango kwa nguvu
'paaaa'
Edna akiwa pale chini na
mwanae ambae hadi wakati huo alikuwa hana fahamu alilia kwa uchungu lakini
hakuna mtu yoyote aliyejali, alimwinua mtoto wake na kumbeba
"Sijui nifanyeje mungu
wangu,sina hata hela ya kumpeleka mtoto hospitali!"
aliwaza huku machozi
yakizidi kumbubujika lakini safari hayakuonekana kwani yalimezwa na maji ya
mvua yaliyokwisha kumlowesha mwili mzima. akaanza kutembea akielekea asikokujua
sababu hakuwa na wazo la kuelekea kwa ndugu, jamaa wala jirani. kitendo chake
cha aibu alichomtendea mumewe kilimfanya auonee aibu ulimwengu wake wote
"Bora kufa tu"
Aliwaza lakini alipofikiria
wazo hilo alijikuta anahairisha wazo lake hilo kwani alijua kwa kufanya hivyo
angemfanya mtoto wake aishi kwa taabu sana.
Bado mvua ilikuwa ikinyesha
hali iliyomfanya Edna aanze kutetemeka kwa baridi , alimfunika mtoto wake na
kitenge ili kumkinga na baridi lakini kitenge hicho hakikufaa chochote kwani
kilikuwa kimelowa chepechepe.
"Koh,koh!"
Dany alikohoa Edna
alishtuka
"Dany, Dany!"
alimwita huku akimtikisa
"Koh, koh"
alikohoa tena
"Dany, Dany"
aliita tena
"mama,mama"
Dany aliita baada ya
kufumbua macho
"Dany , Dany
mwanangu!"
aliita kwa furaha huku
akimkumbatia mwanae
"mgongo unaniuma
mama"
aliongea dany kinyonge
"oh, pole
mwnangu!"
aliongea kwa huruma
"mama kwanini baba
ametufanyia hivi?"
aliuliza, badala ya kujibu
Edna alianza kulia
"usilie mama , niambie
kwanini mama"
alizidi kubembeleza
"Mwanangu baba yako
hana makosa"
aliongea huku akijifuta
machozi kwa kiganja cha mkono wake.
"Hana makosa!! sasa
mbona ametufukuza?"
Dany aliuliza , badala ya
kujibu Edna alianza kulia tena. alijisikia aibu kumweleza mwanae upuuzi
alioufanya, kumsaliti mume wake kwa kutembea na mfanyakazi wake wa kukata nyasi
za n'gombe tena kwenye kitanda anacholala na mumewe
"Hapana mwanangu baba
yako hana makosa kabisa"
Aliongea huku akilia kwa
uchungu , maumivu aliyoyapata moyoni yalimfanya ashindwe kujizuia kulia mbele
ya mwanae.
"Usilie mama"
aliongea Dany kwa huruma
"Acha nilie mwanangu
nina haki ya kulia "
Aliongea Edna huku
akiendeleza kilio chake
"Lakini mama kama baba
hana makosa kwanini unalia sasa?"
aliuliza
"Mimi ndio nina makosa
mwanangu, nimemkosea baba yako!"
aliongea kwa ujasiri huku
bado machozi yakimtoka
"kwanini usimwombe
msamaha?"
"hawezi kunisamehe
mwanangu"
"kwanini kwani
umefanya nini?"
"We acha tu
mwanangu"
"kwanini mama?"
Alizidi kudadisi
"mwanangu hupaswi
kujua, we fahamu kwamba mimi ndio mwenye makosa"
"sasa mama tunaenda
wapi huku?"
"Hata mimi sijui
mwanangu"
"Kama hujui mama
kwanini tusirudi nyumbani?"
"Kule sio kwetu tena
mwanangu."
"sio kwetu!?"
"Ndio mwanagu"
"Kwa nini mama?"
"sababu yule sio baba
yako."
"sio baba yangu!
kivipi?"
"elewa hivyo mwanangu
, baba yako alikwisha kufa"
"Kweli mama? sasa
kwanini haukuniambia toka zamani?"
"acha maswali
mwanangu, nachokueleza ndio hicho"
"sawa mama basi
niambie tunaenda wapi"
"Hayo niachie mimi
mwanangu"
"sawa mama"
aliitikia huku akitetemeka
kutokana na kulowa pamoja na baridi kali la usiku huo.
Maskini Edna alimfariji tu
mwanae, lakini ukweli ni kwamba hata yeye mwenyewe hakujua alikokuwa anaelekea
usiku huo. Kamwe hakuwai kufikiria kama vitendo vyake vingeweza kumuingiza
mwanae katika matatizo, alifikiri kwamba ngeweza kufanya mambo yake bila mumewe
kujua lakini leo bila ya kutahamaki anajikuta katika arobaini yake.
Ukarimu wa Joel
ulimpumbaza, toka alipomuokota akiwa ametupwa barabarani na wanaume walio
mlaghai kwamba wanataka kumnunua alipokuwa akijiuza viwanja na badala yake
wakambaka wakiwa ishirini na kumtupa akiwa amezirai.
Alimpeleka hospitali na
kumlipia matibabu.
Alipomuuliza sehemu
anayoishi hakusita kumweleza kwamba anaishi kwenye ghetto na lundo la wanawake
wenzake . Joel alimuonea huruma na kumpa hifadhi.
Hata alipogunduika kwamba
ana uja uzito kutokana na kubakwa na wale wanaume
Joel alikuwa tayari
kumsaidia kumlea mtoto huyo.
Ni kwa kipindi hicho ndip
joel alipopendekeza kwamba waoane , Edna hakuweza kupinga jambo hilo japo
moyoni alikuwa ajaridhia kuwa na joel.
Alitaka mwanae awe na
maisha bora na Joel ndio alikuwa mwanaume pekee ambaye angeweza kumpatia mwanae
maisha hayo.
Maisha yao yalikuwa ya
furaha kwani Edna lakini huyu kijana wa kazi alipokuja katika
maisha yao ndio alileta mabadiliko katika maisha yao.
Edna hakuweza tena kuizuia
nafsi yake na wala hakujali juu ya mwanae tena alikuwa kama mwendawazimu wa
mapenzi ambaye haambiliki kwa lolote kila mumewe akitoka alikuwa akimlazimisha
kijana huyo wafanye mapenzi kwa kutmia
cheo chake cha ubosi . mpaka siku hiyo walipofumaniwa na Joel alipoamua kuvunja
ukarimu wake wote.
“ nimejichimbia shimo mimi
mwenye”
Aliwaza.
"acha maswali
mwanangu, nachokueleza ndio hicho"
"sawa mama basi niambie
tunaenda wapi"
"Hayo niachie mimi
mwanangu"
"sawa mama"
aliitikia huku akitetemeka
kutokana na kulowa pamoja na baridi kali la usiku huo.
Maskini Edna alimfariji tu
mwanae, lakini ukweli ni kwamba hata
yeye mwenyewe hakujua alikokuwa anaelekea usiku huo. Kamwe hakuwai kufikiria
kama vitendo vyake vingeweza kumuingiza mwanae katika matatizo, alifikiri
kwamba ngeweza kufanya mambo yake bila mumewe kujua lakini leo bila ya
kutahamaki anajikuta katika arobaini yake.
Ukarimu wa Joel
ulimpumbaza, toka alipomuokota akiwa ametupwa barabarani na wanaume walio
mlaghai kwamba wanataka kumnunua alipokuwa akijiuza viwanja na badala yake
wakambaka wakiwa ishirini na kumtupa akiwa hana fahamu.
Alimpeleka hospitali na
kumlipia matibabu.
Alipomuuliza sehemu anayoishi
hakusita kumweleza kwamba anaishi kwenye ghetto na lundo la wanawake wenzake .
Joel alimuonea huruma na kumpa hifadhi.
Hata alipogunduika kwamba
ana uja uzito kutokana na kubakwa na wale wanaume
Joel alikuwa tayari
kumsaidia kumlea mtoto huyo.
Ni kwa kipindi hicho
ndipo joel alipopendekeza kwamba waoane
, Edna hakuweza kupinga jambo hilo japo moyoni alikuwa haja ridhia kuwa na
joel.
Alitaka mwanae awe na
maisha bora na Joel ndio alikuwa mwanaume pekee ambaye angeweza kumpatia mwanae
maisha hayo.
Maisha yao yalikuwa ya
furaha kwani Edna lakini huyu kijana wa kazi alipokuja katika
maisha yao ndio alileta mabadiliko katika maisha yao.
Edna hakuweza tena kuizuia
nafsi yake na wala hakujali juu ya mwanae tena alikuwa kama mwendawazimu wa
mapenzi, ambaye haambiliki kwa lolote kila mumewe akitoka alikuwa akimlazimisha
kijana huyo wafanye mapenzi kwa kutmia
cheo chake cha ubosi . mpaka siku hiyo walipofumaniwa na Joel alipoamua kuvunja
ukarimu wake wote.
“ nimejichimbia shimo mimi
mwenye”
Aliwaza Edna
***
WIKI MOJA BAADAE:
Buguruni sukita kwenye
ghorofa moja bovu, Edna alikuwa amelala
juu ya viroba na maboksi aliyoyatandika kwenye sakafu katika moja ya vyumba vya
ghorofa hilo, alikuwa amejikunyata akikohoa na kutetemeka kwa vichomi
"Dany!, Dany!"
aliita kwa sauti ya kichovu
huku akipata tabu kwa homa kali aliyokuwa nayo. Dany hakuwepo karibu nae na
wala hakuwepo eneo hilo kabisa. Kati kati ya soko la buguruni ndiko Dany
alikokuwa akiangaika huku na kule akiwaomba wapita njia wamsaidie chochote ili akale
na mama yake.
"We mtoto vipi
nimekwambia sina mbona unaning’ang’ania!?"
msichana mmoja aliyevalia
mavazi ya kileo maarufu kama sister du alimkalipia Dany alipokuwa alipokuwa
akimbembeleza ili amsaidie chochote.kilicho mchanganya dany ulikuwa ni muda,
mchana ulikuwa umepita sasa ni jioni lakini hakuna alichokipata zaidi ya maneno
makali toka kwa watu waliokuwa bize na shughuli zao.
hakutia chochote kinywani
mwake wala kumpelekea chochote mama yake. alitembea kinyonge miguu ilikuwa
imeishiwa nguvu sababu ya njaa kali iliyokuwa imembana siku hiyo.
alichoka akaamua kukaa chini jirani kabisa na pipa moja la
kutupia taka huku akisikilizia maumivu makali ya tumbo lililokuwa likimsokota
kwa njaa.
Dada mmoja aliyekuwa
amevalia mavazi ya upishi alimpita Dany akiwa amebeba beseni, alielekekea moja
kwa moja mpaka lilipo pipa la taka.
alipofika pipani alimwaga
kilichokuwemo ndani ya beseni , Macho na Mate yalimtoka Dany kwa tamaa baada ya
kuona kile kilicho mwagwa kwenye pipa hilo. yalikuwa ni mabaki ya vyakula ;
"Hii ndio riziki yangu
leo!"
Dany aliwaza na kuinuka
toka pale chini alipokuwa amekaa. lakini kabla ajapiga hatua yoyote kuelekea
kwenye pipa hilo alishtuka kumuona mbwa mweusi akilivamia pipa hilo na kuanza
kuyafakamia mabaki hayo ya chakula, Dany alichanganyikiwa hakuelewa ni wapi
mbwa huyo alikotokea.
"Haiwezekani !!!"
aliropoka hakuwa tayari
kukikosa chakula hicho sababu aliamini hili ndilo tumaini lake pekee. aliinama
chini na kuokota mawe alianza kumrushia mbwa huyo huku akimpigia kelele za
kumfukuza
"TOKA! TOKAA!"
alimtisha mbwa huyo huku
akizidi kumrushia mawe na michanga.
"Bwee, bwee" mbwa
alibweka baada ya jiwe kumpata, Dany alizidi kurusha mawe zaidi
Bwee! bwee!" alibweka
tena lakini safari hii alishindwa kuvumilia bwa huyo alikimbilia kwenye kichochoro,
Dany pasipo kuchelewa alitupa mawe chini na kukimbilia kwenye pipa hilo. haraka
alianza kuokota chakula hicho na kutia kwenye mfuko wa plastiki, hakujali
takataka zingine zilizokuwamo kwenye pipa hilo zikinuka, alipomaliza aliufunga
mfuko wake na kuelekea alikomuacha mama yake.
Akiwa katika korido la
jengo hilo alisikia sauti ya mama yake ikimuita huku akilalamika kwa maumivu.
"Dany, Dany!"
"Mama nimerudi
mama"
aliitikia na kuingia ndani
ya chumba hicho alichokuwemo mama yake.
"mama!"
"Dany, mh Dany
mwanangu!"
Edna aliongea kwa taabu
"Naam mama nikuletea
chakula"
Aliongea Dany huku
akimsogelea mama yake mpaka pale alipokuwa amelala, huku bado akiwa ameshikilia
mfuko wake wa chakula.alikaachini na kumuinua kichwa mama yake ili aweze kula
kirahisi.
"Chakula mama"
"Dany, Dany
mwanangu"
aliongea kwa taabu
"Naam mama"
"Sijisikii kula
mwanangu!"
"kwanini? haujala toka
jana!"
"Kweli mwanangu sijala
lakini sijisikii kula"
"Mama inatakiwa
ujitahidi"
"Hapana mwanangu siwezi, siwezi kabisa"
"Hapana mwanangu siwezi, siwezi kabisa"
alisisitiza
"Mama bila kula
hauwezi kupona"
aliongea Dany kwa sauti ya
kubembeleza.
"Mwanangu najua
unanipenda mama yako na unataka nipone lakini siwezi Dany,siwezi kula
mwanangu!"
aliongea Edna kwa shida.
jambo hilo lilimuweka Dany katika wakati mgumu sana, hakuwa tayari kumuona mama
yake akishinda na njaa wakati chakula kipo. alijua kuwa mama yake ni mgonjwa na
ajapata tiba yoyote ile hadi wakati huo. walishakwenda hospitali siku za
mwanzoni lakini madaktari waligoma kumpatia tiba sababu hakuwa na pesa, Gesti
walikokuwa wanalala siku za mwanzo nako walifukuzwa sababu hiyo hiyo ya pesa.
walipoomba msaada hakuna mtu aliyewasikiliza shida zao, katika kuhangaika huku na kule ndipo
walipojikuta katika jengo hilo bovu. na hapo ndipo Edna akawa hajiwezi kabisa
hawezi hata kutembea kutwa anashinda amelala, ni kwa wakati huo ndipo mambo
yakabadilika majukumu ya Edna kwa mwanae yakawa ya mwanae kwake, bila ya Dany
kuhangaika kutwa kuomba msaada kwa watu basi walishinda na njaa.
Dany aliangaika akipigwa na jua kutwa na
wakati mwingine kunyeshewa na mvua na alichokipata ndicho alichokula na mama
yake,na hata akikosa iliwabidi kulala na njaa.
Leo baada ya kuangaika bila
mafanikio analazimika kuokota mabaki ya chakula katika pipa la taka tena kwa
kugombaniana na mbwa mweusi, ili walau apate chochote yeye na mama yake, lakini
ajabu mama anakataa kula tena katakata.
"Mama jitahidi hata
kidogo"
alizidi kumbembeleza.
"hapana mwanangu
siwezi kabisa"
"Mama kula japo
kidogo"
Dany alizidi kumbembeleza ,
huku machozi yakimlenga, aliamini chakula ni muhimu sana kwa mama yake kwa
wakati huo.
"Dany mwanangu, najua
unanipenda sana mwanangu, nasikitika mama yako nipo katika hali mbaya sana,
sijui kama kweli naweza kuendelea kuishi"
aliongea kwa taabu.
"hapana mama usiseme
hivyo unajua bado nakuitaji"
"Naju mwanangu ,
nasikitika kukuacha katika hali hii"
"hauwezi kuniacha mama utapona tu"
"Mwananu sina ujanja
tena, najua nakuacha katika hali mbaya sana, la-la-ki-ki-ni sina jinsi
utanisamehe mwanangu ni makosa yangu , makosa yangu ndio yamekufanya uishi kwa
taabu nisamehe mwanangu"
"usiseme hivyo
mama"
Dany aliongea huku machozi
yakimtoka,hali ya mama yake ya sasa ilimtisha.
"Dany da- da-ny
mwa-na-ngu"
anaongoea kwa tabu
"mama"
Dany aliita
"da-da-ny, da-ny"
aliongea huku akitapatapa,
macho yalimtoka kama vile yanataka kugeuka
"Mama,ma"
Dany aliita kwa woga
"mwa- mwa-
na-ngu"
anaita na kukatisha kauli
yake na kisha kutulia kimya
"Mama, mama"
Dany aliita lakini mama
yake bado alikuwa kimya ajibu kitu wala kutikisika
"Mama mama"
Dany aliendelea kuita huku
akimtikisa lakini wapi, hakukuwa na dalili yoyote yakuamka wala kutikisika
'AMEKUFA'
ndicho alichokigundua Dany.
alie na nani msiba huu, amwite nani awe
msaada kwake, mtoto mdogo uskani wa
maisha kaushika mwenyewe hakuna mama wala baba, hakuna mlezi yoyote yule katika
maisha yake.
'HIVI NDIVYO ALIVYOKUWA
MTOTO WA MTAA'.
USIHOFU KILA KITU
KITAKUWA SAWA
Serikali ilipata taarifa juu ya kifo cha mwanamke ,
aliyekuwa akiishi na mwanae katika jumba bovu. Walipomuuliza mtoto huyo juu ya ndugu yoyote anayefahamiana
naye , alijibu hapana.
Ilibidi maiti ya Edna izikwe na manispaa, bila ya msiba,
katika mazishi Danny alikuwa amesimama peke yake akiangalia mwili wa mama yake
ukitumbukizwa katika kaburi.
Alitakiwa kulia lakini mtoto huyu alilia kupita kiasi siku
iliyopita, mpaka machozi yalikauka.
“Pole sana , Danny “
Aliongea mwanaume mmoja aliye mshika bega, aligeuka
kumuangalia mwanume huyo na kumshangaa sababu yeye ndiyo mtu pekee alifika
kumfariji, haukuna mtu yoyote aliyejali juu ya yake kabla na hata hivyo
alimuita jina lake hilo nalo lilimfanya azidi kujiuliza maswali zaidi kuhusu
mwanaume huyo.
“labda alisikia nilpokuwa na hojiwa”
Aliwaza huku akimwa ngalia mwanaume huyo aliyekuwa amesimama
hatua chache toka alipokuwepo yeye.
“ahsante.”
Aliitikia,
“usihofu kila kitu kitakuwa sawa”
Alizidi kumfariji mwanaume huyo, lakini safari hii
alimshangaza, pale alipomwambia kila kitu kitakuwa sawa , wakati kwa alicho
kifahamu yeye ni kwamba kila kitu kitaenda kombo zaidi ya kilivyokuwa awali.
maiti ilikwisha tumbukizwa ndani ya kaburi na kaburi
lilianza kufukiwa, danny aliwaangalia wale watu waliokuwa wakifukia kwa huzuni
kisha akageuka kumuangalia Yule mtu aliyekuwa akimfariji, wala hakuwepo pale
alipokuwa amesimama awali, alijaribu kupepeasa macho yake kila sehemu katika
maeneo hayo ya makaburi lakini hakuona hata dalili ya kuwepo mwanaume huyo
mahali, hapo. Danny alibaki ameduwaa. Muda si mrefu alibaki yeye na kabuli la
mama yake. Safari hii machozi yalianza
kumtoka upya alishika udongo uliokuwa uliokuwa juu ya kaburi hilo huku akilia
kwa uchungu.
Ilimuumiza kuona ndugu pekee aliyekuwa nae kamwe hawezi
kufumbua mdomo wake na kutoa kauli yoyote kwake.
“natakiwa kusonga mbele “
Aliwaza na kisha akaumwaga udongo aliokuwa ameushikilia
mikononi. Akisimama wima na kuianza safari, safari ambayo hata yeye mwenyewe
hakujua muelekeo wake, inatakiwa aende mahali ambapo anaweza kupata chakula na
ukifika usiku alale, hakutaka kurejea tena kwenye lile jengo bovu ambalo yeye
pamoja na mama yake walikuwa wakikaa, alijua mazingira yale yata mfanya
akumbuke mengi kuhusu mama yake jambo ambalo litamfanya ashinde akilia wakati
wote.
**********------------***********
Miezi miwili na wiki tatu zilikwisha katika tangu Danny ,
ampoteze mama yake, katika kipindi chote
hicho bado kula yake ilikuwa ni
kuomba omba kwa wapita njia katika kila kona ya jiji. Lakini hali ilikuwa ngumu
mno kwani watu wengi walikuwa wakiwa puuzia watoto wa mtaani na kuwaona kama
uchafu Fulani katika jiji.
“Baba ! Baba!”
Danny aliita mara baada ya kukutana ana kwa ana na Jerry,
wakati alipokuwa akiomba omba katika mgari yaliyokuwa katika foleni.hii ni kwa
mara ya kwanza tangu kifo cha mama yake uso wake kuonyesha tabasamu. Ilikuwa
kama vile amepata tumaini alilokuwa amekwisha kata tama la kulipata tena.
“Wewe chokoraa nani baba yako, una kichaa”
Aliongea Jerry kwa kufoka. Danny alishangaa hakujua kama
mbaka wakati huo Jerry angekuwa na hasira .
“Baba , mama amekufa!”
Aliongea Dannya akijaribu kueleza habari kifo cha Edna
akifiri labda Jerry atamuonea huruma.
“wewe mwendawazi usieleze upuuzi wako, sina undugu na
takataka kama wewe”
Alifoka .
“nionee huruma baba sina mahali pa kuishi, nateseka sana”
“wewe mwendawazimu, unafikiri unaweza kuingia nyumba ya nani
ulivyo hivyo
Wewe ni mtoto wa mtaa tu, sahau habari mahali pa kuishi,
mama yako hakukueleza ukweli,
Alibakwa na wahuni kibao ndio ukapatikana wewe, hivyo kaa
ukijua hapo ndio nyumbani kwenu, wewe ni mwana haramu, mtoto wa mtaa kwa damu
kabisa, baba zako ndio hao hao wahuni waliopo huko mtaani na mama yako alikuwa
Malaya kama ulikuwa hujui, niijaribu kumpa maisha ili aishi na kama watu
wengine lakini yeye akaamua kunionyesha ukunguru wake.
Acha kabisa kuita ita watu barabarani baba baba, huwezi kuwa
na baba mwenye hadhi .
Huwezi kuishi kama watu wa kawaida wewe ni mtoto wa mtaa
umenielewa , mtoto wa mtaa mwanaharamu mkubwa wewe”
Alifoka Jerry maneno hayo makali yalimfanya Danny atokwe na
machozi mfululizo, kamwe hakuwahi kutegemea kwamba siku moja atakuja kusikia
maneno makali kama hayo kuhusu maisha yake. Tena toka kwa mtu kama jerry ,
alijua kwamba walikorofishana na mama yake lakini hakujua kwamba jerry anaweza
kuwa mtu asiye na moyo wa kibinadamu kama hivyo.
Alichokifanya Jerry ni kufunga kioo cha gari lake na mara
baada ya foleni kuruhusiwa aliliondosha gari lake kama yalivyofanya magari
mengine katika msululu huo .
Danny alitoka pembeni ya barabara na kukaa chini ya nguzo
kubwa iliyobeba bango la matangazo.
Alilia kuliko alivyowahi kulia katika kipindi chochote
katika maisha yake, hata siku ya msiba wa mama yake hakulia kama alivyolia leo.
Hakuwahi kufikiria kabisa kwamba historia ya maisha yake imepinda kiasi hicho. Leo ndio alijua kwamba
baba yake hakufa bali ni mmoja kati wale wanaume watukutu wanaofanya uharifu wa kila aina
katika jiji , pengine hata yeye alikuwa mtoto wa mtaa enzi za utoto wake. Na
juu ya mama yake hilo ndilo lilimuumiza zaidina kujiona mtu mwenye mkosi zaidi
katika ulimwengu huu .
“ kwa nini maisha yangu yamekuwa hivi jamani”
Aliwaza Danny huku machozi yakizidi kumbubujika kama vile
mwenda wazimu.
“hutakiwi kulia, Danny, unahitaji kupambana.”
Danny aliisikia sauti hiyo iliyomshtua kweli kweli, aligeuka
haraka kuangalia mahali ambapo sauti hiyo ilitokea , alimuona mwanaume akiwa
amesimama mbele yake akiwa ameshika mfuko wa plastiki pamoja na kitambaa mkono
mwingine. Mwanaume huyu hakuwa mgeni machoni kwa Danny, alikuwa ni Yule Yule
aliyemshika bega siku ile ya mazishi ya mama yake kule makaburini na kumwambia
asijali kila kitu kitakuwa sawa. Mwanaume huyo alipotea katika kipindi chote
cha miezi miwili naa, leo amesimama mbele yake tena wakati ambapo ana majonzi
kama yale aliyokuwa nayo kipindi kile na anamfariji kama alivyo mfariji wakati
ule.
“wewe ni nani?”
“ hilo halitakusaidia kwa sasa, shika leso ujifute machozi”
Mwanaume huyo aliongea akiwa amemsogelea , ilimuwia vigumu
Danny kumuamini mwanaume huyo lakini ilmbidi kufanya hivyo kwa kuwa huyo ndiye
mtu peke aliye na kitu ambacho alikuwa akikiitaji sana kwa wakati huo ,
‘Faraja’
“nimekuletea chakula na maji najua una njaa”
Aliongea mwanaume huyo na kumpatia mfuko wa plastiki
aliokuwa ameushika, Danny aliufungua, ulikuwa na take away pamoja na maji ya
kopo.”
“Ahsante”
Danny alishukuru
“Usijali”
Mwanaume huyo aliitikia
kisha akanyanyuka na kuanza kuondoka.
“Unaondoka?” Danny aliliza
“ Niamini Danny bado unahitaji kuwa peke yako”
Aliongea mwanaume huyo na kisha kuendelea kutembea, hatua
kadhaa kando ya barabara kulikuwa na gari ya kifahari aina ya humer Yule
mwanaume aliingia ndani ya gari hilona kisha likaondoka, hilo lilikuwa jambo la
ajabu sana kwa Danny alibaki ameduwaa kwa sekunde kadhaa, huyo mwanaume hakuwa mtu aliyemuonea huruma
na kumsaidia tu bali alikuwa ni mtu aliyekuwa akifika wakati ule ambao Danny
alikuwa akihitaji kuwa na mtu.
“ ni nani huyu ?”
Danny aliwaza, lakini hakupata jibu lolote hata habari
aliyokuwa ikimtoa machozi dakika kumi na tano zilizopita haikuwa na uzito tena
, aliwisha rudia katika hali yake ya awali.
***
TUMCHOME
MOTO
Wiki mbili baadae
Katika mtaa Danny
alikuwa anakimbia huku akiwa ameshika mfuko wenye mkate, huku watu wakimbiza, alikimbia kadri ya uwezo
wake , na huku watu anao mfukuza wakizidi kuongezeka
“MWIZI !, MWIZI!”
Walipiga yowe watu hao huku wakimkimbiza, wengine
walimrushia mawe , na wengine wakiwa
wameshika mapanga na marungu na siraha zingine zote za jadi unazozijua
wewe .
Danny alikimbia kadri ya uwezo wake lakini watu walio ibuka
katika kila kichochoro cha mtaa aliopita wwalizidi kumkaribia.
“ Mungu naomba unisaidie”
Aliwaza danny hku akizidi kukimbia, mwanaume mmoja
aliyetokea mbele yake na alimkata mtama, Danny anadondoka huku akibilingika
chini mfululizo.
Alijaribu kunyanyuka tena lakini ikashindikana baada ya jiwe
kutua mgongoni kwake na kumfanya adondoke chini tena.
Sekunde kidogo watu tayari walikuwa wamesha mzunguka, hawakujali umri wa mtoto huyo,
walimpiga kila mtu kwa namna anavyojisikia.
“TUMCHOME MOTO”
Mmoja kati ya watu hao alilopoka.
“ kweli kabisa , hawa chokoraa wamezidi kwa udokozi”
“watakuja kutushikia mitutu baadae tukiwaachia”
Waliongea watu hao, bila huruma yoyote , maskini Danny nja
ndio iliyomfanya aukwapue mkate huo kwenye duka na Mangi.
Kutwa nzima alikuwa akizunguka katika mitaa akioma lakini
watu wote walikuwa wakimpuuzia.
Alijutia uamuzi wake wa kunyosha mkono katika duka lile na
kuunyofoa mkate huo, hakujua kwamba tendo dogo kama hilo lingeweza kuyagharimu
maisha yake yote.
Alibaki akilia tu huku damu zikimtoka katika maeneo mbali
mbali ambayo watu walimjeruhi kwa kumbonda na mawe. Gurudumu la gari likaletwa
na wakamvisha kisha wakaanza kumwagia mafuta aina ya petroli
“hii ndio jeuri yao wana haramu hawa “
Mmoja kati ya watu hao aliropoka huku wengine wakishangilia,
huku wakiwa na shauku kubwa ya kuona tukio hilo la kinyama. Mioyo yao
hata haikuwa suto ya kwamba kwamba huyo
ni binadamu mwenzao tena mtoto mdogo.
“WOO, WOO WOOO”
Kilisikika king’ora cha gari la polisi likija kwa kasi
katika eneo hilo, kila mmoja alibaki ameduwaa
Kwani jambo hilo halikuwa la kawaida kutokea katika mtaa huo
, mara nyingi ving’ora vilisikika kama kuna msafara wa raisi ama FFU wakiwa
katika oparesheni yao ya kutuliza ghasia na kweli leo walikuwa ni FFU , hakuna
aliyejuwa askari hao walichokifuata ila walishangaa kuona askari hao wakiruka
kwenye gari hata kabla gari hilo halijasimama wakiwa wamevalia mavazi yao ya
kazi na virungu vyao. mabomu ya machozi yalirushwa na watu wakaanza kutwangwa
virungu.
Kila mmoja alikimba alikokujua. Lakini cha moto
alikiona kwa mong’oto mkali toka kwa
askali hao.
Danny alikuwa hoi pale chini. Tayari alikwisha Sali sala
yake ya mwisho na alijua hatima ya maisha yake imekwisha timia lakini badala
yake aliona watu wakitawanyika kwa kukimbia huku na kule, huku moshi uliokuwa
ukiwafanya watu watokwe machozi ukiwa umetanda. Japo macho yake yalikuwa yakitoka
machozi lakini alifanikiwa kuliona gai
nyeusi aina ya humer iliyokuwa imeegeshwa pembeni kidogo na eneo la tukio hilo
lilipofanyika. macho yake hayakuweza kuona tena na hata hivyo hali yake ilikuwa mbaya
zaidi kutokana na kipigo kikali alichokipata kutoka kwa raia wenye hasira kali.
Akajikuta anadondoka chini na akiwa ajitambui askali mmoja alimbeba na kisha
wakamwingiza katika gari ya wagonjwa iliyokuwa imeegeshwa pembeni .
“Kapoteza fahamu
kabisa”
aliongea mmoja kati
ya watabibu waliokuwemo ndani ya gari hilo la wagonjwa akiongea na Yule
mwanaume aliye kutana na Danny mara kadhaa akiwa na matatizo.
“mnatakiwakufanya kadri ya uwezo wenu kuhakikisha anapona,
mnajua jinsi mtoto huyu alivyo na umuhimu mkubwa kwangu”
Mwanaume huyo aliongea.
“Ndio mheshimiwa, tutajitahidi sana”
Aliitikia mtabibu huyo na gari hilo liliondolewa kwa kasi
likipiga king’ora cha kuashilia wamebeba mgonjwa mahututi.
“Hii serikali imechanganyikiwa, yani imetucharaaza virungu
mtaa mzima kwa ajili ya chokoraa!”
Aliongea mmoja kati ya watu waliokuwa katika tukio hilo
akiwa hoi bin taaabani kutokana na mkon’goto alioupata kutoka kwa Askali hao wa
kutuliza Ghasia.
Hilo lilikuwa ni tukio la aina yake katika mtaa huo, kamwe
hawakuwahi kuona serikali wala tasisi yoyote ile ikionyesha kujali Mtoto wa
mtaani kama ambavyo walishuhudia siku hiyo.
***
Gari la wagonjwa lilinyooka moja kwa moja mpaka katika
hospitali ya Aga khan. Lilposimama tu . haraka walimshusha Danny na kumpakia
katika tololi la kubebea wagonjwa akiwa na dripu ya maji ambayo walimfunga toka
akiwa ndani ya gari moja kwa moja walimpeleka katika chumba cha wagonjwa
mahututi.
Yule mwanaume alikuwa amesimama nje ya chumba hicho
akisubiri majibu kutoka kwa watabibu hao ambao walikuwa wakimshughulikia Danny
kadri wawezavyo.
Baada ya muda kidogo mganga alitoka nje, mwanaume huyo
akamfuata.
“daktari”
“hauhitaji kuwa na shaka tena bw. Jacob, kila kitu kimeenda
sawa hana maumivu ya ndani ni kuvuja damu tu kutokana na majeraha aliyoyapata
ndio kumemfanya awe katika hali kama hiyo lakini hadi wakati huu maisha yake
hayapo kwenye hatari tena, anachohitaji ni matibabu ya siku kadhaa, kwa ajili ya majeraha yake alafu atarejea
katika hali yake ya kawaida .”
“ inaweza kuchukua muda gani?”
“Siku kumi hadi kumi na tano”
“ahsante daktari”
“karibu.”
Aliongea Daktari huyo na kisha akaondoka na kumuacha Jacob,
akiwa ameketi katika Benchi.
Simu yake iliita , akaipokea.
“Tumefikia wapi?”
ilisikika sauti toka kwenye simu ikiuliza.
“Opareshini imefanikiwa, mheshimiwa, mtoto yupo salama”
Aliitikia.
“kazi nzuri, nakuhitaji makao makuu sasa”
“ndiyo, mheshimiwa.”
Alikata simu na kisha kuelekea katika gari lake. Aliliwasha
na kisha kuliondoa kwa kasi.
***
Danny alishtuka toka usingizini na kuhema kwa kasi .
“ MSINIUE, MSINIUE! MIMI
SIO MWIZI NAOMBA MSINIUE! “
Danny aliongea maneno hayo mfululizo mara baada ya kushtuka,
nesi alikimbia haraka mpaka kwenye kitanda chake na kumshika.
“Tulia, Tulia, upo sehemu salama, hakuna atakaye kuua!”
Nesi huyo alijaribu kumtuliza lakini Danny bado alikua
akikukuruka. Ukweli ni kwamba mtoto huyu alikuwa amwaini mtu yoyote sasa hivi.
“MSINIUE, TAFADHARI, USINIUE!”
Alizidi kupiga yowe.
“Tulia , tulia tafadhari , unahitaji kutulia”
Nesi huyo alizidi kumtuliza lakini Danny hakuwezakufanya
hivyo.
“Kimetokea nini!”
Daktari aliuiza mara baada ya kuingia ndani ya chumba hicho
haraka.
“HEE WANAZIDI KUONGEZEKA, WANATA KA KUNI CHOMA MOTO, JAMA
MIMI SIO MWIZI JAMANI , NIACHENI MIMI
TAFADHARI, NI MTOTO WA MTAANI TU NILIKUWA
NA NJAA JAMANI MSINICHOME MOTO”
“tulia afadhari tulia , hatukuui tuna kusaidia.
Tulia”
Aliongea daktari akisaidiana na nesi lakini wapi danny
alikuwa amecharuka kabisa, alichokitaka kwa wakati huo ni kuchoropoka mikononi
mwao.
“ is not going to come down , I need a sedative right the
way!” ( atoweza kutulia nahitaji dawa ya usingizi haraka sana!)
Aliongea daktari huyo kwa msisitizo.
“ yes sir” ( ndiyo
mheshimiwa )
Aliitikia muuguzi huyo na kukimbia mpaka kwenye duka la
dawa.
.”Subi, I need a sedative right a way we got an emergency
in 444.”
( Subi nahitaji dawa ya usingizi haraka sana tuna dharula
chumba namba 444 )
Aliongea mara baada ya kufika kwenye duka hilo
“you got it” ( umepata)
Muuzaji wa dawa aliitikia na kisha kumpatia dawa akampa
kitabu akasini haraka na kisha akaaanza kukimbia tena.
“MSINIUE NIACHENI MIMI MISNIUE”
Zilisikika kelele za Danny mara bada ya nesi huyo kuingia,
hakuamini alichoiona alikuta dokta na Danny wakiwa kwemye kona ya chumba hicho
daktari akijaribu kumbana Danny na Danny akijaribu kujichoropoa mikononi mwake.
“ what the hell are you waiting for give him a shot right now”
( unasubiria nini?, mchome sasa hivi) daktari alifoka na
kumfanya nesi aliyekuwa ameduwaa akimbie haraka na kumchoma Danny sindano.
Na hapo hapo alitulia na kulala kabisa , ilibaki kazi ya
kumbeba na kumpandisha kitandani.
Kwa pamoja walisaidiana na kumlaza kisha wote waIichoka hoi
hoi.
MWISHO WA KITABU CHA 1
No comments:
Post a Comment