GIFT KIPAPA

Thursday, July 7, 2016

MTOTO WA MTAA BOOK 1







BY D.G.LWASYE 'GIFT KIPAPA'

MBEBE MWANAO MTOKE
Mvua kumbwa iliyoambatana na miungurumo ya radi ilikuwa ikinyesha,
 mishale ya saa tatu za za usiku karibu kila mtu alikuwa amejifungia nyumbani kwake akiutafuta usingizi katika usiku huo uliokuwa na kibaridi.
"Mamaaaaaaaa!!!!!!"
Ilisikika sauti hiyo ya mtoto akilia maeneo ya tabata bima jijini dar es salaam.
"Utaniua mume wangu!"
Mwanamke alisikika akilia kwa uchungu huku sauti za mikanda na mabao zikisikika
"Baba muache mama!"
Mtoto aliongea huku akilia kwa uchungu
"Kelele wewe mwana haramu, mimi sio baba yako!"
Aliongea mwanaume huyo huku akimwangalia mtoto huyo kwa ghadhabu.
"mume wangu jamani!!"
Mwanamke aliongea kwa sauti ya kinyonge
"Pumbavu na wewe kimya malaya mkumbwa"
Aliongea huku akimgeukia mwanamke huyo na kisha kumpiga teke zito la tumboni
'Puuuuu'
"Uuuuh"
Mwanamke alilia kwa uchungu
"Nitakuua leo malaya mkubwa wewe"
aliongea kwa ukali huku akimshushia mvua ya mikanda mwanamke huyo
"Nisamehe mume wangu mwanamke alilalamika lakini badala ya kumhurumia mwanaume huyo ndio kwanza alizidi kupandwa na hasira, alizidi kumpiga huku akitoa matusi ya nguoni
"Malaya mkumbwa wewe leo utanikoma!"
"Baba muache mama, baba naomba babaa"
Mtoto alizidi kuangua kilio lakini mwanaume huyo
hakujali kauli hiyo ya mtoto, aliendelea tu kumpiga mwanamke.
Mtoto alishindwa kuvumilia akaenda kumvaa mwilini baba yake.
"Baba muache mama , baba muache, ba....."
Alilia mtoto huyo kwa uchungu huku akiwa ameishikilia miguu ya baba yake akimsihi aache kumpiga mama yake.
"Pumbavu mwana haramu weee!!"
aliongea mwanaume huyo na kisha kumbutua mtoto huyo kama mpira mpaka kudondokea kwenye meza iliyokuwa sentimita kadhaa toka pale walipokukuwa
"Mungu wangu!!!!"
aliongea kwa mshituko mwanamke baada ya kushuudia kitendo hicho cha kinyama alihisi uchungu wote wa uzazi umejirudia hakuwai kumuona mwanae akiviringika kiasi hicho
"Kelele usiniite tena mumeo mimi sio mumeo!"
Aliongea kwa ukali na kuanza tena kumshambulia mwanamke huyo kwa mateke na mangumi.
"Baa,ba...."
Mtoto alitaka kuongea lakini alitaka kuongea
lakini alishindwa kutokana na maumivu makali aliyoyapata alipoangukia kwenye meza
"Dany!,Dany!"
Mwanamke aliita huku akimwangalia mtoto.
"Mama,ma!"
Mtoto nae aliita lakini kwa taabu na kisha kudondoka chini
"Dany! ,Dany!"
Mwanamke aliita lakini mtoto hakuitika wala kutikisika pale chini alipodondokea.
"Mmume wangu Dany ame...."
Alikatishwa na bao zito lililotua usoni kwake.
"Nimekwishakueleza mimi sio mume wako"
aliongea mwanaume huyo kwa ukali
"Lakini mtoto amezimia Joel!"
Aliongea mwanamke huyo kwa sauti ya upole
"Kwahiyo kama amezimia?"
Aliuliza kwa dharau
"Joel kama makosa nimefanya mimi na sio mtoto"
Mwanamke huyo alizidi kuongea kwa huruma
"Hilo mimi sijali wewe na mtoto wako wote sitaki kuwaona"
"Joel jamani!!"
"Joel nini? Beba hicho kipaka chako utoke nyumbani kwangu sasa hivi"
Aliongea kwa ukali
"Joel jamani!! nisamehe"
"Hakuna cha msamaha hapa nimeshasema toka!"
Alisisitiza na kuanza kumsukuma mwanamke huyo ili atoke
"Joel jamani mvua inanyesha alafu usiku saa hizi"
aliongea mwanamke huyo kwa huruma
"Usinieleze habari za mvua mimi nimesema mbebe mwanao mtoke"
alisisitiza mwanaume huyo kwa ukali, uso wake hakuonyesha hata chembe ya huruma
"Toka usikii?" alizidi kufoka
"Joel muonee huruma mtoto mvua hii"
"Mtoto nini mpeleke kwa baba yake, nimesema mtoke"
alizidi kufoka huku akimsukumiza, mwanamke huyo alijisogeza mpaka alipo mwanae na kujaribu kumwinua
"Dany, Dany!"
Aaliiita huku akimtikisa mtoto
"Nimesema toka Edna nikizidi kusikia hilo jina la kitoto chako unazidi kunichefua, toka unisikii?"
alifoka Joel huku akimsukuma Edna.
"Joel jamani kuwa Binadamu, mvua yote hii kweli tutoke?"
Edna alijaribu kumbembeleza
"ubinadamu! unaujua ubinadamu wewe? ungekuwa binadamu ungenifanyia yote haya?"
aliongea Joel kwa ukali
"Najua Joel ndio maana nakuomba msamaha, naomba Joel mvua hii muonee huruma mtoto"
"Mtoto!, mtoto nini si wako nimesema tokaaaaa"
alizidi kufoka na kuendelea kumsukumiza, alifungua mlango na kumsukumia nje
"Joel jamani tuhurumie"
aliongea kwa huruma baada ya Joel kumsukumiza nje kwenye mvua, yeye na mtoto wake walidondoka chini kwenye matope
 'pwaaaa'
"tokaaaaaaa!"
Joel alifoka na kisha kuubamiza mlango kwa nguvu
'paaaa'
Edna akiwa pale chini na mwanae ambae hadi wakati huo alikuwa hana fahamu alilia kwa uchungu lakini hakuna mtu yoyote aliyejali, alimwinua mtoto wake na kumbeba
"Sijui nifanyeje mungu wangu,sina hata hela ya kumpeleka mtoto hospitali!"
aliwaza huku machozi yakizidi kumbubujika lakini safari hayakuonekana kwani yalimezwa na maji ya mvua yaliyokwisha kumlowesha mwili mzima. akaanza kutembea akielekea asikokujua sababu hakuwa na wazo la kuelekea kwa ndugu, jamaa wala jirani. kitendo chake cha aibu alichomtendea mumewe kilimfanya auonee aibu ulimwengu wake wote
"Bora kufa tu"
Aliwaza lakini alipofikiria wazo hilo alijikuta anahairisha wazo lake hilo kwani alijua kwa kufanya hivyo angemfanya mtoto wake aishi kwa taabu sana.

Bado mvua ilikuwa ikinyesha hali iliyomfanya Edna aanze kutetemeka kwa baridi , alimfunika mtoto wake na kitenge ili kumkinga na baridi lakini kitenge hicho hakikufaa chochote kwani kilikuwa kimelowa chepechepe.
"Koh,koh!"
Dany alikohoa Edna alishtuka
"Dany, Dany!"
alimwita huku akimtikisa
"Koh, koh"
alikohoa tena
"Dany, Dany"
aliita tena
"mama,mama"
Dany aliita baada ya kufumbua macho
"Dany , Dany mwanangu!"
aliita kwa furaha huku akimkumbatia mwanae
"mgongo unaniuma mama"
aliongea dany kinyonge
"oh, pole mwnangu!"
aliongea kwa huruma
"mama kwanini baba ametufanyia hivi?"
aliuliza, badala ya kujibu Edna alianza kulia
"usilie mama , niambie kwanini mama"
alizidi kubembeleza
"Mwanangu baba yako hana makosa"
aliongea huku akijifuta machozi kwa kiganja cha mkono wake.
"Hana makosa!! sasa mbona ametufukuza?"
Dany aliuliza , badala ya kujibu Edna alianza kulia tena. alijisikia aibu kumweleza mwanae upuuzi alioufanya, kumsaliti mume wake kwa kutembea na mfanyakazi wake wa kukata nyasi za n'gombe tena kwenye kitanda anacholala na mumewe
"Hapana mwanangu baba yako hana makosa kabisa"
Aliongea huku akilia kwa uchungu , maumivu aliyoyapata moyoni yalimfanya ashindwe kujizuia kulia mbele ya mwanae.
"Usilie mama"
aliongea Dany kwa huruma
"Acha nilie mwanangu nina haki ya kulia "
Aliongea Edna huku akiendeleza kilio chake
"Lakini mama kama baba hana makosa kwanini unalia sasa?"
aliuliza
"Mimi ndio nina makosa mwanangu, nimemkosea baba yako!"
aliongea kwa ujasiri huku bado machozi yakimtoka
"kwanini usimwombe msamaha?"
"hawezi kunisamehe mwanangu"
"kwanini kwani umefanya nini?"
"We acha tu mwanangu"
"kwanini mama?"
Alizidi kudadisi
"mwanangu hupaswi kujua, we fahamu kwamba mimi ndio mwenye makosa"
"sasa mama tunaenda wapi huku?"
"Hata mimi sijui mwanangu"
"Kama hujui mama kwanini tusirudi nyumbani?"
"Kule sio kwetu tena mwanangu."
"sio kwetu!?"
"Ndio mwanagu"
"Kwa nini mama?"
"sababu yule sio baba yako."
"sio baba yangu! kivipi?"
"elewa hivyo mwanangu , baba yako alikwisha kufa"
"Kweli mama? sasa kwanini haukuniambia toka zamani?"
"acha maswali mwanangu, nachokueleza ndio hicho"
"sawa mama basi niambie tunaenda wapi"
"Hayo niachie mimi mwanangu"
"sawa mama"
aliitikia huku akitetemeka kutokana na kulowa pamoja na baridi kali la usiku huo.

Maskini Edna alimfariji tu mwanae, lakini ukweli ni kwamba hata yeye mwenyewe hakujua alikokuwa anaelekea usiku huo. Kamwe hakuwai kufikiria kama vitendo vyake vingeweza kumuingiza mwanae katika matatizo, alifikiri kwamba ngeweza kufanya mambo yake bila mumewe kujua lakini leo bila ya kutahamaki anajikuta katika arobaini yake.
Ukarimu wa Joel ulimpumbaza, toka alipomuokota akiwa ametupwa barabarani na wanaume walio mlaghai kwamba wanataka kumnunua alipokuwa akijiuza viwanja na badala yake wakambaka wakiwa ishirini na kumtupa akiwa amezirai.
Alimpeleka hospitali na kumlipia matibabu.
Alipomuuliza sehemu anayoishi hakusita kumweleza kwamba anaishi kwenye ghetto na lundo la wanawake wenzake . Joel alimuonea huruma na kumpa hifadhi.
Hata alipogunduika kwamba ana uja uzito kutokana na kubakwa na wale wanaume
Joel alikuwa tayari kumsaidia kumlea mtoto huyo.

Ni kwa kipindi hicho ndip joel alipopendekeza kwamba waoane , Edna hakuweza kupinga jambo hilo japo moyoni alikuwa ajaridhia kuwa na joel.
Alitaka mwanae awe na maisha bora na Joel ndio alikuwa mwanaume pekee ambaye angeweza kumpatia mwanae maisha hayo.
Maisha yao yalikuwa ya furaha  kwani Edna  lakini huyu kijana wa kazi alipokuja katika maisha yao ndio alileta mabadiliko katika maisha yao.
Edna hakuweza tena kuizuia nafsi yake na wala hakujali juu ya mwanae tena alikuwa kama mwendawazimu wa mapenzi ambaye haambiliki kwa lolote kila mumewe akitoka alikuwa akimlazimisha kijana huyo wafanye mapenzi  kwa kutmia cheo chake cha ubosi . mpaka siku hiyo walipofumaniwa na Joel alipoamua kuvunja ukarimu wake wote.
“ nimejichimbia shimo mimi mwenye”
Aliwaza.  
"acha maswali mwanangu, nachokueleza ndio hicho"
"sawa mama basi niambie tunaenda wapi"
"Hayo niachie mimi mwanangu"
"sawa mama"
aliitikia huku akitetemeka kutokana na kulowa pamoja na baridi kali la usiku huo.

Maskini Edna alimfariji tu mwanae,  lakini ukweli ni kwamba hata yeye mwenyewe hakujua alikokuwa anaelekea usiku huo. Kamwe hakuwai kufikiria kama vitendo vyake vingeweza kumuingiza mwanae katika matatizo, alifikiri kwamba ngeweza kufanya mambo yake bila mumewe kujua lakini leo bila ya kutahamaki anajikuta katika arobaini yake.
Ukarimu wa Joel ulimpumbaza, toka alipomuokota akiwa ametupwa barabarani na wanaume walio mlaghai kwamba wanataka kumnunua alipokuwa akijiuza viwanja na badala yake wakambaka wakiwa ishirini na kumtupa akiwa hana fahamu.
Alimpeleka hospitali na kumlipia matibabu.
Alipomuuliza sehemu anayoishi hakusita kumweleza kwamba anaishi kwenye ghetto na lundo la wanawake wenzake . Joel alimuonea huruma na kumpa hifadhi.
Hata alipogunduika kwamba ana uja uzito kutokana na kubakwa na wale wanaume
Joel alikuwa tayari kumsaidia kumlea mtoto huyo.
Ni kwa kipindi hicho ndipo  joel alipopendekeza kwamba waoane , Edna hakuweza kupinga jambo hilo japo moyoni alikuwa haja ridhia kuwa na joel.
Alitaka mwanae awe na maisha bora na Joel ndio alikuwa mwanaume pekee ambaye angeweza kumpatia mwanae maisha hayo.
Maisha yao yalikuwa ya furaha  kwani Edna  lakini huyu kijana wa kazi alipokuja katika maisha yao ndio alileta mabadiliko katika maisha yao.
Edna hakuweza tena kuizuia nafsi yake na wala hakujali juu ya mwanae tena alikuwa kama mwendawazimu wa mapenzi, ambaye haambiliki kwa lolote kila mumewe akitoka alikuwa akimlazimisha kijana huyo wafanye mapenzi  kwa kutmia cheo chake cha ubosi . mpaka siku hiyo walipofumaniwa na Joel alipoamua kuvunja ukarimu wake wote.
“ nimejichimbia shimo mimi mwenye”
Aliwaza Edna



   ***


WIKI MOJA BAADAE:
Buguruni sukita kwenye ghorofa moja bovu, Edna  alikuwa amelala juu ya viroba na maboksi aliyoyatandika kwenye sakafu katika moja ya vyumba vya ghorofa hilo, alikuwa amejikunyata akikohoa na kutetemeka kwa vichomi
"Dany!, Dany!"
aliita kwa sauti ya kichovu huku akipata tabu kwa homa kali aliyokuwa nayo. Dany hakuwepo karibu nae na wala hakuwepo eneo hilo kabisa. Kati kati ya soko la buguruni ndiko Dany alikokuwa akiangaika huku na kule akiwaomba wapita njia wamsaidie chochote ili akale na mama yake.
"We mtoto vipi nimekwambia sina mbona unaning’ang’ania!?"
msichana mmoja aliyevalia mavazi ya kileo maarufu kama sister du alimkalipia Dany alipokuwa alipokuwa akimbembeleza ili amsaidie chochote.kilicho mchanganya dany ulikuwa ni muda, mchana ulikuwa umepita sasa ni jioni lakini hakuna alichokipata zaidi ya maneno makali toka kwa watu waliokuwa bize na shughuli zao.
hakutia chochote kinywani mwake wala kumpelekea chochote mama yake. alitembea kinyonge miguu ilikuwa imeishiwa nguvu sababu ya njaa kali iliyokuwa imembana siku hiyo.
alichoka akaamua  kukaa chini jirani kabisa na pipa moja la kutupia taka huku akisikilizia maumivu makali ya tumbo lililokuwa likimsokota kwa njaa.
Dada mmoja aliyekuwa amevalia mavazi ya upishi alimpita Dany akiwa amebeba beseni, alielekekea moja kwa moja mpaka lilipo pipa la taka.
alipofika pipani alimwaga kilichokuwemo ndani ya beseni , Macho na Mate yalimtoka Dany kwa tamaa baada ya kuona kile kilicho mwagwa kwenye pipa hilo. yalikuwa ni mabaki ya vyakula ;
"Hii ndio riziki yangu leo!"
Dany aliwaza na kuinuka toka pale chini alipokuwa amekaa. lakini kabla ajapiga hatua yoyote kuelekea kwenye pipa hilo alishtuka kumuona mbwa mweusi akilivamia pipa hilo na kuanza kuyafakamia mabaki hayo ya chakula, Dany alichanganyikiwa hakuelewa ni wapi mbwa huyo alikotokea.
"Haiwezekani !!!"
aliropoka hakuwa tayari kukikosa chakula hicho sababu aliamini hili ndilo tumaini lake pekee. aliinama chini na kuokota mawe alianza kumrushia mbwa huyo huku akimpigia kelele za kumfukuza
"TOKA! TOKAA!"
alimtisha mbwa huyo huku akizidi kumrushia mawe na michanga.
"Bwee, bwee" mbwa alibweka baada ya jiwe kumpata, Dany alizidi kurusha mawe zaidi
Bwee! bwee!" alibweka tena lakini safari hii alishindwa kuvumilia bwa huyo alikimbilia kwenye kichochoro, Dany pasipo kuchelewa alitupa mawe chini na kukimbilia kwenye pipa hilo. haraka alianza kuokota chakula hicho na kutia kwenye mfuko wa plastiki, hakujali takataka zingine zilizokuwamo kwenye pipa hilo zikinuka, alipomaliza aliufunga mfuko wake na kuelekea alikomuacha mama yake.
Akiwa katika korido la jengo hilo alisikia sauti ya mama yake ikimuita huku akilalamika kwa maumivu.
"Dany, Dany!"
"Mama nimerudi mama"
aliitikia na kuingia ndani ya chumba hicho alichokuwemo mama yake.
"mama!"
"Dany, mh Dany mwanangu!"
Edna aliongea kwa taabu
"Naam mama nikuletea chakula"
Aliongea Dany huku akimsogelea mama yake mpaka pale alipokuwa amelala, huku bado akiwa ameshikilia mfuko wake wa chakula.alikaachini na kumuinua kichwa mama yake ili aweze kula kirahisi.
"Chakula mama"
"Dany, Dany mwanangu"
aliongea kwa taabu
"Naam mama"
"Sijisikii kula mwanangu!"
"kwanini? haujala toka jana!"
"Kweli mwanangu sijala lakini sijisikii kula"
"Mama inatakiwa ujitahidi"
"Hapana mwanangu siwezi, siwezi kabisa"
alisisitiza
"Mama bila kula hauwezi kupona"
aliongea Dany kwa sauti ya kubembeleza.
"Mwanangu najua unanipenda mama yako na unataka nipone lakini siwezi Dany,siwezi kula mwanangu!"
aliongea Edna kwa shida. jambo hilo lilimuweka Dany katika wakati mgumu sana, hakuwa tayari kumuona mama yake akishinda na njaa wakati chakula kipo. alijua kuwa mama yake ni mgonjwa na ajapata tiba yoyote ile hadi wakati huo. walishakwenda hospitali siku za mwanzoni lakini madaktari waligoma kumpatia tiba sababu hakuwa na pesa, Gesti walikokuwa wanalala siku za mwanzo nako walifukuzwa sababu hiyo hiyo ya pesa. walipoomba msaada hakuna mtu aliyewasikiliza shida zao,  katika kuhangaika huku na kule ndipo walipojikuta katika jengo hilo bovu. na hapo ndipo Edna akawa hajiwezi kabisa hawezi hata kutembea kutwa anashinda amelala, ni kwa wakati huo ndipo mambo yakabadilika majukumu ya Edna kwa mwanae yakawa ya mwanae kwake, bila ya Dany kuhangaika kutwa kuomba msaada kwa watu basi walishinda na njaa.
 Dany aliangaika akipigwa na jua kutwa na wakati mwingine kunyeshewa na mvua na alichokipata ndicho alichokula na mama yake,na hata akikosa iliwabidi kulala na njaa.
Leo baada ya kuangaika bila mafanikio analazimika kuokota mabaki ya chakula katika pipa la taka tena kwa kugombaniana na mbwa mweusi, ili walau apate chochote yeye na mama yake, lakini ajabu mama anakataa kula tena katakata.
"Mama jitahidi hata kidogo"
alizidi kumbembeleza.
"hapana mwanangu siwezi kabisa"
"Mama kula japo kidogo"
Dany alizidi kumbembeleza , huku machozi yakimlenga, aliamini chakula ni muhimu sana kwa mama yake kwa wakati huo.
"Dany mwanangu, najua unanipenda sana mwanangu, nasikitika mama yako nipo katika hali mbaya sana, sijui kama kweli naweza kuendelea kuishi"
aliongea kwa taabu.
"hapana mama usiseme hivyo unajua bado nakuitaji"
"Naju mwanangu , nasikitika kukuacha katika hali hii"
"hauwezi kuniacha  mama utapona tu"
"Mwananu sina ujanja tena, najua nakuacha katika hali mbaya sana, la-la-ki-ki-ni sina jinsi utanisamehe mwanangu ni makosa yangu , makosa yangu ndio yamekufanya uishi kwa taabu nisamehe mwanangu"
"usiseme hivyo mama"
Dany aliongea huku machozi yakimtoka,hali ya mama yake ya sasa ilimtisha.
"Dany da- da-ny mwa-na-ngu"
anaongoea kwa tabu
"mama"
Dany aliita
"da-da-ny, da-ny"
aliongea huku akitapatapa, macho yalimtoka kama vile yanataka kugeuka
"Mama,ma"
Dany aliita kwa woga
"mwa- mwa- na-ngu"
anaita na kukatisha kauli yake na kisha kutulia kimya
"Mama, mama"
Dany aliita lakini mama yake bado alikuwa kimya ajibu kitu wala kutikisika
"Mama mama"
Dany aliendelea kuita huku akimtikisa lakini wapi, hakukuwa na dalili yoyote yakuamka wala kutikisika
'AMEKUFA'
ndicho alichokigundua Dany.  alie na nani msiba huu, amwite nani awe msaada kwake,  mtoto mdogo uskani wa maisha kaushika mwenyewe hakuna mama wala baba, hakuna mlezi yoyote yule katika maisha yake.
'HIVI NDIVYO ALIVYOKUWA MTOTO WA MTAA'.

                                                        


USIHOFU KILA KITU KITAKUWA SAWA

Serikali ilipata taarifa juu ya kifo cha mwanamke , aliyekuwa akiishi na mwanae katika jumba bovu. Walipomuuliza  mtoto huyo juu ya ndugu yoyote anayefahamiana naye , alijibu hapana.
Ilibidi maiti ya Edna izikwe na manispaa, bila ya msiba, katika mazishi Danny alikuwa amesimama peke yake akiangalia mwili wa mama yake ukitumbukizwa  katika kaburi.
Alitakiwa kulia lakini mtoto huyu alilia kupita kiasi siku iliyopita, mpaka machozi yalikauka.
“Pole sana , Danny “
Aliongea mwanaume mmoja aliye mshika bega, aligeuka kumuangalia mwanume huyo na kumshangaa sababu yeye ndiyo mtu pekee alifika kumfariji, haukuna mtu yoyote aliyejali juu ya yake kabla na hata hivyo alimuita jina lake hilo nalo lilimfanya azidi kujiuliza maswali zaidi kuhusu mwanaume huyo.
“labda alisikia nilpokuwa na hojiwa”
Aliwaza huku akimwa ngalia mwanaume huyo aliyekuwa amesimama hatua chache toka alipokuwepo yeye.
“ahsante.”
Aliitikia,
“usihofu kila kitu kitakuwa sawa”
Alizidi kumfariji mwanaume huyo, lakini safari hii alimshangaza, pale alipomwambia kila kitu kitakuwa sawa , wakati kwa alicho kifahamu yeye ni kwamba kila kitu kitaenda kombo zaidi ya kilivyokuwa awali.
maiti ilikwisha tumbukizwa ndani ya kaburi na kaburi lilianza kufukiwa, danny aliwaangalia wale watu waliokuwa wakifukia kwa huzuni kisha akageuka kumuangalia Yule mtu aliyekuwa akimfariji, wala hakuwepo pale alipokuwa amesimama awali, alijaribu kupepeasa macho yake kila sehemu katika maeneo hayo ya makaburi lakini hakuona hata dalili ya kuwepo mwanaume huyo mahali, hapo. Danny alibaki ameduwaa. Muda si mrefu alibaki yeye na kabuli la mama yake.  Safari hii machozi yalianza kumtoka upya alishika udongo uliokuwa uliokuwa juu ya kaburi hilo huku akilia kwa uchungu.
Ilimuumiza kuona ndugu pekee aliyekuwa nae kamwe hawezi kufumbua mdomo wake na kutoa kauli yoyote kwake.
“natakiwa kusonga mbele “
Aliwaza na kisha akaumwaga udongo aliokuwa ameushikilia mikononi. Akisimama wima na kuianza safari, safari ambayo hata yeye mwenyewe hakujua muelekeo wake, inatakiwa aende mahali ambapo anaweza kupata chakula na ukifika usiku alale, hakutaka kurejea tena kwenye lile jengo bovu ambalo yeye pamoja na mama yake walikuwa wakikaa, alijua mazingira yale yata mfanya akumbuke mengi kuhusu mama yake jambo ambalo litamfanya ashinde akilia wakati wote.
                                   
                                 **********------------***********

Miezi miwili na wiki tatu zilikwisha katika tangu Danny , ampoteze mama yake, katika kipindi chote  hicho bado kula yake ilikuwa  ni kuomba omba kwa wapita njia katika kila kona ya jiji. Lakini hali ilikuwa ngumu mno kwani watu wengi walikuwa wakiwa puuzia watoto wa mtaani na kuwaona kama uchafu Fulani katika jiji.
“Baba ! Baba!”
Danny aliita mara baada ya kukutana ana kwa ana na Jerry, wakati alipokuwa akiomba omba katika mgari yaliyokuwa katika foleni.hii ni kwa mara ya kwanza tangu kifo cha mama yake uso wake kuonyesha tabasamu. Ilikuwa kama vile amepata tumaini alilokuwa amekwisha kata tama la kulipata tena.
“Wewe chokoraa nani baba yako, una kichaa”
Aliongea Jerry kwa kufoka. Danny alishangaa hakujua kama mbaka wakati huo Jerry angekuwa na hasira .
“Baba , mama amekufa!”
Aliongea Dannya akijaribu kueleza habari kifo cha Edna akifiri labda Jerry atamuonea huruma.
“wewe mwendawazi usieleze upuuzi wako, sina undugu na takataka kama wewe”
Alifoka .
“nionee huruma baba sina mahali pa kuishi, nateseka sana”
“wewe mwendawazimu, unafikiri unaweza kuingia nyumba ya nani ulivyo hivyo
Wewe ni mtoto wa mtaa tu, sahau habari mahali pa kuishi, mama yako hakukueleza ukweli,
Alibakwa na wahuni kibao ndio ukapatikana wewe, hivyo kaa ukijua hapo ndio nyumbani kwenu, wewe ni mwana haramu, mtoto wa mtaa kwa damu kabisa, baba zako ndio hao hao wahuni waliopo huko mtaani na mama yako alikuwa Malaya kama ulikuwa hujui, niijaribu kumpa maisha ili aishi na kama watu wengine lakini yeye akaamua kunionyesha ukunguru wake.
Acha kabisa kuita ita watu barabarani baba baba, huwezi kuwa na baba mwenye hadhi .
Huwezi kuishi kama watu wa kawaida wewe ni mtoto wa mtaa umenielewa , mtoto wa mtaa mwanaharamu mkubwa wewe”
Alifoka Jerry maneno hayo makali yalimfanya Danny atokwe na machozi mfululizo, kamwe hakuwahi kutegemea kwamba siku moja atakuja kusikia maneno makali kama hayo kuhusu maisha yake. Tena toka kwa mtu kama jerry , alijua kwamba walikorofishana na mama yake lakini hakujua kwamba jerry anaweza kuwa mtu asiye na moyo wa kibinadamu kama hivyo.
Alichokifanya Jerry ni kufunga kioo cha gari lake na mara baada ya foleni kuruhusiwa aliliondosha gari lake kama yalivyofanya magari mengine katika msululu huo .
Danny alitoka pembeni ya barabara na kukaa chini ya nguzo kubwa iliyobeba bango la matangazo.
Alilia kuliko alivyowahi kulia katika kipindi chochote katika maisha yake, hata siku ya msiba wa mama yake hakulia kama alivyolia leo. Hakuwahi kufikiria kabisa kwamba historia ya maisha yake  imepinda kiasi hicho. Leo ndio alijua kwamba baba yake hakufa bali ni mmoja kati wale wanaume  watukutu wanaofanya uharifu wa kila aina katika jiji , pengine hata yeye alikuwa mtoto wa mtaa enzi za utoto wake. Na juu ya mama yake hilo ndilo lilimuumiza zaidina kujiona mtu mwenye mkosi zaidi katika ulimwengu huu .
“ kwa nini maisha yangu yamekuwa hivi jamani”
Aliwaza Danny huku machozi yakizidi kumbubujika kama vile mwenda wazimu.
“hutakiwi kulia, Danny, unahitaji kupambana.”
Danny aliisikia sauti hiyo iliyomshtua kweli kweli, aligeuka haraka kuangalia mahali ambapo sauti hiyo ilitokea , alimuona mwanaume akiwa amesimama mbele yake akiwa ameshika mfuko wa plastiki pamoja na kitambaa mkono mwingine. Mwanaume huyu hakuwa mgeni machoni kwa Danny, alikuwa ni Yule Yule aliyemshika bega siku ile ya mazishi ya mama yake kule makaburini na kumwambia asijali kila kitu kitakuwa sawa. Mwanaume huyo alipotea katika kipindi chote cha miezi miwili naa, leo amesimama mbele yake tena wakati ambapo ana majonzi kama yale aliyokuwa nayo kipindi kile na anamfariji kama alivyo mfariji wakati ule.
“wewe ni nani?”
“ hilo halitakusaidia kwa sasa, shika leso ujifute machozi”
Mwanaume huyo aliongea akiwa amemsogelea , ilimuwia vigumu Danny kumuamini mwanaume huyo lakini ilmbidi kufanya hivyo kwa kuwa huyo ndiye mtu peke aliye na kitu ambacho alikuwa akikiitaji sana kwa wakati huo , ‘Faraja’
“nimekuletea chakula na maji najua una njaa”
Aliongea mwanaume huyo na kumpatia mfuko wa plastiki aliokuwa ameushika, Danny aliufungua, ulikuwa na take away pamoja na maji ya kopo.”
“Ahsante”
Danny alishukuru
“Usijali”
Mwanaume huyo aliitikia  kisha akanyanyuka na kuanza kuondoka.
“Unaondoka?” Danny aliliza
“ Niamini Danny bado unahitaji kuwa peke yako”
Aliongea mwanaume huyo na kisha kuendelea kutembea, hatua kadhaa kando ya barabara kulikuwa na gari ya kifahari aina ya humer Yule mwanaume aliingia ndani ya gari hilona kisha likaondoka, hilo lilikuwa jambo la ajabu sana kwa Danny alibaki ameduwaa kwa sekunde kadhaa,  huyo mwanaume hakuwa mtu aliyemuonea huruma na kumsaidia tu bali alikuwa ni mtu aliyekuwa akifika wakati ule ambao Danny alikuwa akihitaji kuwa na mtu.
“ ni nani huyu ?”
Danny aliwaza, lakini hakupata jibu lolote hata habari aliyokuwa ikimtoa machozi dakika kumi na tano zilizopita haikuwa na uzito tena , aliwisha rudia katika hali yake ya awali.



***












TUMCHOME MOTO

Wiki mbili baadae
Katika mtaa  Danny alikuwa anakimbia huku akiwa ameshika mfuko wenye mkate,  huku watu wakimbiza, alikimbia kadri ya uwezo wake , na huku watu anao mfukuza wakizidi kuongezeka
“MWIZI !, MWIZI!”
Walipiga yowe watu hao huku wakimkimbiza, wengine walimrushia mawe , na wengine wakiwa  wameshika mapanga na marungu na siraha zingine zote za jadi unazozijua wewe .
Danny alikimbia kadri ya uwezo wake lakini watu walio ibuka katika kila kichochoro cha mtaa aliopita wwalizidi kumkaribia.
“ Mungu naomba unisaidie”
Aliwaza danny hku akizidi kukimbia, mwanaume mmoja aliyetokea mbele yake na alimkata mtama, Danny anadondoka huku akibilingika chini mfululizo.
Alijaribu kunyanyuka tena lakini ikashindikana baada ya jiwe kutua mgongoni kwake na kumfanya adondoke chini tena.
Sekunde kidogo watu tayari walikuwa wamesha  mzunguka, hawakujali umri wa mtoto huyo, walimpiga kila mtu kwa namna anavyojisikia.
“TUMCHOME MOTO”
Mmoja kati ya watu hao alilopoka.
“ kweli kabisa , hawa chokoraa wamezidi kwa udokozi”
“watakuja kutushikia mitutu baadae tukiwaachia”
Waliongea watu hao, bila huruma yoyote , maskini Danny nja ndio iliyomfanya aukwapue mkate huo kwenye duka na Mangi.
Kutwa nzima alikuwa akizunguka katika mitaa akioma lakini watu wote walikuwa wakimpuuzia.
Alijutia uamuzi wake wa kunyosha mkono katika duka lile na kuunyofoa mkate huo, hakujua kwamba tendo dogo kama hilo lingeweza kuyagharimu maisha yake yote.
Alibaki akilia tu huku damu zikimtoka katika maeneo mbali mbali ambayo watu walimjeruhi kwa kumbonda na mawe. Gurudumu la gari likaletwa na wakamvisha kisha wakaanza kumwagia mafuta aina ya petroli
“hii ndio jeuri yao wana haramu hawa “
Mmoja kati ya watu hao aliropoka huku wengine wakishangilia, huku wakiwa na   shauku kubwa  ya kuona tukio hilo la kinyama. Mioyo yao hata haikuwa suto ya kwamba  kwamba huyo ni binadamu mwenzao tena mtoto mdogo.

“WOO, WOO WOOO”

Kilisikika king’ora cha gari la polisi likija kwa kasi katika eneo hilo, kila mmoja alibaki ameduwaa
Kwani jambo hilo halikuwa la kawaida kutokea katika mtaa huo , mara nyingi ving’ora vilisikika kama kuna msafara wa raisi ama FFU wakiwa katika oparesheni yao ya kutuliza ghasia na kweli leo walikuwa ni FFU , hakuna aliyejuwa askari hao walichokifuata ila walishangaa kuona askari hao wakiruka kwenye gari hata kabla gari hilo halijasimama wakiwa wamevalia mavazi yao ya kazi na virungu vyao. mabomu ya machozi yalirushwa na watu wakaanza kutwangwa virungu.
Kila mmoja alikimba alikokujua. Lakini cha moto alikiona  kwa mong’oto mkali toka kwa askali hao.
Danny alikuwa hoi pale chini. Tayari alikwisha Sali sala yake ya mwisho na alijua hatima ya maisha yake imekwisha timia lakini badala yake aliona watu wakitawanyika kwa kukimbia huku na kule, huku moshi uliokuwa ukiwafanya watu watokwe machozi ukiwa umetanda. Japo macho yake yalikuwa yakitoka machozi lakini alifanikiwa  kuliona gai nyeusi aina ya humer iliyokuwa imeegeshwa pembeni kidogo na eneo la tukio hilo lilipofanyika. macho yake hayakuweza kuona tena     na hata hivyo hali yake ilikuwa mbaya zaidi kutokana na kipigo kikali alichokipata kutoka kwa raia wenye hasira kali. Akajikuta anadondoka chini na akiwa ajitambui askali mmoja alimbeba na kisha wakamwingiza katika gari ya wagonjwa iliyokuwa imeegeshwa pembeni .    
     “Kapoteza fahamu kabisa”
 aliongea mmoja kati ya watabibu waliokuwemo ndani ya gari hilo la wagonjwa akiongea na Yule mwanaume aliye kutana na Danny mara kadhaa akiwa na matatizo.
“mnatakiwakufanya kadri ya uwezo wenu kuhakikisha anapona, mnajua jinsi mtoto huyu alivyo na umuhimu mkubwa kwangu”
Mwanaume huyo aliongea.
“Ndio mheshimiwa, tutajitahidi sana”
Aliitikia mtabibu huyo na gari hilo liliondolewa kwa kasi likipiga king’ora cha kuashilia wamebeba mgonjwa mahututi.
“Hii serikali imechanganyikiwa, yani imetucharaaza virungu mtaa mzima kwa ajili ya chokoraa!”
Aliongea mmoja kati ya watu waliokuwa katika tukio hilo akiwa hoi bin taaabani kutokana na mkon’goto alioupata kutoka kwa Askali hao wa kutuliza Ghasia.
Hilo lilikuwa ni tukio la aina yake katika mtaa huo, kamwe hawakuwahi kuona serikali wala tasisi yoyote ile ikionyesha kujali Mtoto wa mtaani kama ambavyo walishuhudia siku hiyo.

***
Gari la wagonjwa lilinyooka moja kwa moja mpaka katika hospitali ya Aga khan. Lilposimama tu . haraka walimshusha Danny na kumpakia katika tololi la kubebea wagonjwa akiwa na dripu ya maji ambayo walimfunga toka akiwa ndani ya gari moja kwa moja walimpeleka katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Yule mwanaume alikuwa amesimama nje ya chumba hicho akisubiri majibu kutoka kwa watabibu hao ambao walikuwa wakimshughulikia Danny kadri  wawezavyo.
Baada ya muda kidogo mganga alitoka nje, mwanaume huyo akamfuata.
“daktari”
“hauhitaji kuwa na shaka tena bw. Jacob, kila kitu kimeenda sawa hana maumivu ya ndani ni kuvuja damu tu kutokana na majeraha aliyoyapata ndio kumemfanya awe katika hali kama hiyo lakini hadi wakati huu maisha yake hayapo kwenye hatari tena, anachohitaji ni matibabu ya siku kadhaa,  kwa ajili ya majeraha yake alafu atarejea katika hali yake ya kawaida .”
“ inaweza kuchukua muda gani?”
“Siku kumi hadi kumi na tano”
“ahsante daktari”
“karibu.”
Aliongea Daktari huyo na kisha akaondoka na kumuacha Jacob, akiwa ameketi katika Benchi.
Simu yake iliita , akaipokea.
“Tumefikia wapi?”
ilisikika sauti toka kwenye simu ikiuliza.
“Opareshini imefanikiwa, mheshimiwa, mtoto yupo salama”
Aliitikia.
“kazi nzuri, nakuhitaji makao makuu sasa”
“ndiyo, mheshimiwa.”

Alikata simu na kisha kuelekea katika gari lake. Aliliwasha na kisha kuliondoa kwa kasi.

***

Danny alishtuka toka usingizini na kuhema kwa kasi .
“ MSINIUE, MSINIUE! MIMI  SIO MWIZI NAOMBA   MSINIUE! “
Danny aliongea maneno hayo mfululizo mara baada ya kushtuka, nesi alikimbia haraka mpaka kwenye kitanda chake na kumshika.
“Tulia, Tulia, upo sehemu salama, hakuna atakaye kuua!”
Nesi huyo alijaribu kumtuliza lakini Danny bado alikua akikukuruka. Ukweli ni kwamba mtoto huyu alikuwa amwaini mtu yoyote sasa hivi.
“MSINIUE, TAFADHARI, USINIUE!”
Alizidi kupiga yowe.
“Tulia , tulia tafadhari , unahitaji kutulia”
Nesi huyo alizidi kumtuliza lakini Danny hakuwezakufanya hivyo.
“Kimetokea nini!”
Daktari aliuiza mara baada ya kuingia ndani ya chumba hicho haraka.
“HEE WANAZIDI KUONGEZEKA, WANATA KA KUNI CHOMA MOTO, JAMA MIMI  SIO MWIZI JAMANI , NIACHENI MIMI TAFADHARI, NI MTOTO WA MTAANI TU NILIKUWA  NA NJAA JAMANI MSINICHOME MOTO”
“tulia afadhari tulia , hatukuui tuna kusaidia.
 Tulia”
Aliongea daktari akisaidiana na nesi lakini wapi danny alikuwa amecharuka kabisa, alichokitaka kwa wakati huo ni kuchoropoka mikononi mwao.
“ is not going to come down , I need a sedative right the way!” ( atoweza kutulia nahitaji dawa ya usingizi haraka sana!)
Aliongea daktari huyo kwa msisitizo.
“ yes sir”  ( ndiyo mheshimiwa )
Aliitikia muuguzi huyo na kukimbia mpaka kwenye duka la dawa.
.”Subi, I need a sedative right a way we got an emergency in  444.”
( Subi nahitaji dawa ya usingizi haraka sana tuna dharula chumba namba 444 )
Aliongea mara baada ya kufika kwenye duka hilo
“you got it” ( umepata)
Muuzaji wa dawa aliitikia na kisha kumpatia dawa akampa kitabu akasini haraka na kisha akaaanza kukimbia tena.
“MSINIUE NIACHENI MIMI MISNIUE”
Zilisikika kelele za Danny mara bada ya nesi huyo kuingia, hakuamini alichoiona alikuta dokta na Danny wakiwa kwemye kona ya chumba hicho daktari akijaribu kumbana Danny na Danny akijaribu kujichoropoa mikononi mwake.
“ what the hell are you waiting for give him a shot  right now”
( unasubiria nini?, mchome sasa hivi) daktari alifoka na kumfanya nesi aliyekuwa ameduwaa akimbie haraka na kumchoma Danny sindano.
Na hapo hapo alitulia na kulala kabisa , ilibaki kazi ya kumbeba na kumpandisha kitandani.
Kwa pamoja walisaidiana na kumlaza kisha wote waIichoka hoi hoi.



MWISHO WA KITABU CHA 1





















No comments:

Post a Comment