MKE WANGU
ANATAKA KUNIUA BOOK 1
By gift
kipapa
KWA UFUPI;
Utafanya
nini endapo ukigundua kwamba Yule unayempenda na kumthamini kuliko kitu
chochote cha maisha yako, ndio mtu hatari zaidi kwako , unalala nae kitanda
kimoja, na unamshirikisha maswala yako yote lakini pale inapofikia hatua ya
mtutu wa bunduki kunyooshewa kwenye paji la uso wako ni yeye ndio anakuwa
amekishika kifyatulio cha risasi, hafanyi mzaha na wewe , bali ni kweli
kabisa amenuia kukumaliza bila shaka
hicho kinaweza kuwa kipindi kigumu zaidi katika maisha yako, simulizi hii
iliyonuia kuugusa moyo mmoja hadi mwingine
imesukwa kwa mara nyingine na
Deogratius gift kipapa Lwasye ili kuongea na moyo wa yoyote huko nje ambaye
yupo katika uhusiano wa kimapenzi na hata aliye nje ya uhusiano.
MWANZO WA
SIMULIZI:
Ni miezi
miwili tu imepita tangu nifunge ndoa. Harusi kubwa ya kifahari iliyokuwa
imesheheni kila aina ya vivutio. Mbali na hayo harusi hiyo kwangu ilikuwa
kutimilika kwa ndoto ya kukamilisha furaha katika maisha yangu kwa kuoa
mwanamke mwenye kila sifa ya uzuri ambao
nilikuwa nataka mke wangu awe nao, alikuwa mzuri sio siri machoni pangu
alionekana kama vile malaika , na kweli
alikuwa , nilipokutana naye kwa mara ya kwanza niliamini ni Mungu
mwenyewe ndio ameamua kunishushia mrembo huyu. Jina lake ni judy , lakini mimi
nilipenda kumuita malaika.
“malaika
wangu.”
“abee , mume
wangu.”
Aliitika.
“nakupenda
sana.”
“Nami
nakupenda pia mume wangu.”
Hivyo ndivyo
mapenzi yetu yalivyokuwa , tulipenda na sana sio siri.
Baada ya
kufunga ndoa yetu tulienda kula fungate yetu nchini Thailand katika jiji la bangkonk. Jiji lililosheheni
kila aina ya starehe. Tukiwa huko siwezi kukuficha jinsi maisha yetu
yalivyokuwa ya furaha.
Tulitembea
katika jiji hilo kama malkia na mfalme tukifurahia vivutio vya mji huo pamoja
na kwenda kwenye vivutio vya kila aina kama vile maporomoko ya maji ya
kushangaza na fukwe za bahari zilizo
sehemu iliyojificha na mambo mengine mengi ambayo hata kuyaelezea siwezi , kwa
kweli ilikuwa furaha tupu. Mpaka tulitamani maisha yetu yote yangekuwa huko.
“mume wangu
, yani nimepapenda kweli hapa.”
“hata mimi
mpenzi lazima tutakuja tena rikizo.”
“kweli?”
“niamini mke wangu.”
“nitashukuru
kweli mume wangu yani.”
“usihofu
mpenzi wewe ni malkia wangu , nitafanya kila kitu , kwa ajili yako.”
“ndio maana
nakupenda honey .”
Aliongea na
kisha kunibusu , na wala halikuwa busu rahisi bali denda , macho yetu yalifumba
tulipokuwa tunyonyana , wala hatukuogopa kufanya hivyo barabarani kwenye umati
wa watu waliokuwa wametingwa wakihangaika na shughuli zao hakuna hata aliyekuwa
na muda wakutuangalia sisi.
“habari ,
ndege wawili , mnataka kunywa damu ya
nyoka .”
Aliongea
mwanume mmojamwenye asili ya huko
aliyesogea karibu yetu na kutufanya tukatishe busu letu.
“damu ya
nyoka!”
“ndio damu
ya nyoka ,kobra, sssssss.”
Aliongea
huku akijaribu kuuchezesha ulimi wake na kutoa sauti ambayo nyoka huwa
wanatoa wakiwa wameutoa ulimi wao.
“hapana , hatuhitaji damu ya nyoka.”
Niliongea .
“kwa nini
mnaogopa , wapendanao wengi wanapenda kunywa, inasemekana mkinywa damu ya nyoka
kwa pamoja mnafanya mapenzi yenu yadumu kwa muda mrefu zaidi.”
Aliongea
mwanaume huyo huku akituangalia usoni.
Na sisi pia
tuliangaliana usoni , kusema kweli hoja yake ilikuwa imetugusa sote ,
hatujawahi kunywa damu ya nyoka na wala hakuna yoyote kati yetu aliyewahi
kufikiria kama siku moja atakuja kunywa kitu kama damu ya nyoka , lakini kwa
ajili ya mapenzi , kwa kweli mtu anaweza kufanya lolote.
“tutakunywa!”
Tulisema kwa
pamoja hadi wenyewe tulijishangaa , kugongana sauti , mwanaume huyo alitupeleka
kwenye chumba hicho ambacho walikuwa wakiiandaa hiyo damu ya nyoka , karibu
chumba kizima kilikuwa kimejaa nyoka aina ya kobra na wengine tofauti tofauti.
SE
Lakini
walikuwa katika masanduku ya vioo ,na katika masanduku hayo muda wote walikuwa
wakitishia kung’ata mtu yoyote aliyeingia kwenye chumba hicho japo waliishia
kuvigonga vioo vya masanduku hayo.
“kwenye meza
ya kupimia hiyo damu ya nyoka kulikuwa na mwanaume mwingine ambaye alimimina
damu hiyo kwenye .
Kweny glasi
ndogo zile zinazotumika kunywea pombe kali baa.
Tulishika
glasi hizo huku tukiangaliana usoni .
“kwa ajili
ya mapenzi yetu.”
Niliongea huku nikimsogezea Judy glasi hiyo ili tugonge chears.
“kwa mapenzi
yetu.”
Naye pia
aliitikia na kisha tuliyagongesha
maglasi hayo na kunywa kwa pamoja .
Sio siri
damu hiyo ilIkuwa chungu, lakini ilitubidi tumeze hivyo hivyo.
Hivyo ndivyo
yalivyokuwa mapenzi yetu huko Bangkok ,
na sasa tupo nyumbani tanzania kwenye makazi yetu Mbezi beach , wiki
moja imesha pita tangu tuwasili kutoka nchini Thailand
***
Ndugu jamaa na marafiki walitupokea kwa
shangwe tuliporejea nchini. Ilifanyika sherehe kubwa nyumbani kwetu, na baadae
sherehe iliamia katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Yani harusi
ni kama vile ilikuwa imefungwa upya, ndugu zangu wote walirejea nyumbani tena
kwa ajili ya kuja kunipokea mimi pamoja na mke wangu , japo nao pia walikuwa
wanatoka nchi mbali mbali, ulikuwa ni utamaduni ya familia yetu.
Hata ukiwa
mbali kiasi gani na uwe umetingwa kaisi gani, ikifanyika shughuli nyumbani basi
lazima uhudhurie, baba yabgu alikuwa mkali sana kwa yoyote anayethubutu kukosa
kuhudhuria.
Hata hivyo
tofauti na shughuli zingine zilizowahi kufanyika katika familia yetu, hii
ilionekana kuwafurahisha zaidi ndugu zangu , nafikiri kwa kuwa nilikuwa mziwanda na kipenzi cha
kila mmoja hata hivyo hii ilikuwa harusi
ya mwisho kufungwa katika familia.
Kaka zangu
wote pamoja na dada tayari walikuwa wamefunga harusi zao , kama miaka mitano
sita hivi iliyopita na wengine walikuwa mpaka na miaka kumi na tano katika
ndoa.
Ukumbini
niliwaarika wafanyakazi wangu wote, siku hiyo ofisi haikufunguliwa kabisa ,
kila mmoja alikuwa hapo kusherekea kurejea kwa bosi.
Na wana familia walichokifanya siku hiyo
kilikuwa cha kushangaza kwa kweli , walianza kutoa zawadi upya kila mmoja
alitoa zaidi ya zile zawadi alizotoa siku ya harusi , ilikuwa ni kufuru kwa
kweli , magari ya kifahari tulimiminiwa kama vile utitiri , yani kama vile
tulikuwa tunapewa mtaji wa kuuza magari.
Na mama
yangu ndio alitia fora zawadi aliyoitoa ilifunika zawadi zote zilizotolewa siku
hiyo na kufanya watu wote washikwe na bumbuwazi.
“sitaki
mwanangu ajibane bane tena atakapokuwa anasafiri , ndege hii binafsi ataitumia
katika safari zake zote akiwa na mkewe.”
Aliongea
mama na watu wote walishangilia , mimi mdomo wangu ulikuwa wazi , nilijua
kwamba mama ananipenda kuliko watoto wake wote lakini sikujua kwamba angeweza
kudiriki kuninunulia ndege yangu mwenyewe .
Ilikuwa ni
model mpya kabisa ya ndege ilikuwa ni ndege ya kifahari yenye injini mbili
model: the new eclipse 550 personal jet.
Gharama yake
ilikuwa ni dola milioni 2.7 na ilikuwa na inakadiriwa kwenda kasi mpaka mph
430.
Hata baba
mwenyewe alishangazwa na zawadi hii , pamoja kushinda nae lakini siri hii
hakumwambia.
Ndugu zangu
wote walibaki wameduwaa. Na kwa mke wangu ndio ilibaki kidogo azimie kwa
mshtuko jambo hili lilikuwa limepitiliza kusema kweli.
Na ilipofika
zamu yangu ya kuongea chochote kwa watu.
Nilishika kipaza
sauti huku nikijidai. Maneno yangu yalikuwa machache lakini yalimgusa kila mtu.
“ninapaswa
kuwashuku watu wote mliopo hapa, lakini mniwie radhi kwa kile ambacho mama
yangu amefanya leo kimeziteka hisia zangu zote. Amenifanya nitambue ya kwamba
yeye si mwanamke aliyebeba kwenye tumbo lake na kisha kunizaa na kunilea mpaka
nilipokuwa mtu mzima na kunicha niende zangu, leo amenithibitishia kwamba ni
mwanamke mwenye uwezo na nguvu za kunilinda katika kipindi chote cha maisha
yangu, ni wangapi kati yenu hapa mama zenu wanaweza kufanya hivyo mnyooshe mikono yenu ili niione.”
Nilipoongea
hivyo kuna baadhi ya watu walinyoosha na wengine walibaki kushangilia tu.
“msidanganye, msidanganye! Sijauliza kwamba wangapi wanapendwa na mama zao, najua kila mama anampenda mwane , nimeuliza ni wangapi mama zenu wana nguvu kama alizo nazo mama yangu, na nitakuamini kama ukinionyesha ndege ya kwako mwenyewe , ambayo umezawadiwa na mama yako. ”
“msidanganye, msidanganye! Sijauliza kwamba wangapi wanapendwa na mama zao, najua kila mama anampenda mwane , nimeuliza ni wangapi mama zenu wana nguvu kama alizo nazo mama yangu, na nitakuamini kama ukinionyesha ndege ya kwako mwenyewe , ambayo umezawadiwa na mama yako. ”
Niliongea
huku watu wakicheka , kwa kweli siku hiyo ilikuwa siku ya kipekee kwangu.
Marafiki
ndugu zangu na wafanyakazi wote wa kampuni yangu walikuwa na furaha kweli siku
hiyo, tulikunywa kadiri tulivyojisikia , tulicheza muziki na kusherekea kwa
kila namna , kwa kweli siku hiyo ilikuwa siku kweli kweli.
Ahsubuhi ya
siku iliyofuata wafanya kazi wangu hawakwenda kazini niliwaamuru wapumzike.
mgazeti
yaliyochapwa siku hiyo yalipabwa picha yangu. Huku yakiwa na vichwa vya habari
vilivyoeleza kunihusu , kila gazeti waliandika kichwa hicho kwa kukipamba kwa
jinsi walivyojua wao.
‘ TAJIRI DEO
AREJEA JIJINI’ ‘ DEO AFANYA KUFURU’ ‘JIJI LAWAKA MOTO KWA MBWE MBWE ZA DON
DEO.’
na vingine vingi wala sikujali picha yangu
kupabwa kwenye magazeti lilikuwa jambo la kawaida , nikionekana kwenye kumbi za
starehe , nikitoa msaada Fulani , nikishinda tenda , nikiwa mgeni rasmi kwenye
hafla Fulani na hata wakati mwingine nikionekana katika maeneo ya uswahilini,
wenyewe waliniita Don lakini
nina hakika
watu hawa hawajui lolote kuhusu ndugu zangu, kwani kila kitu nilicho nacho
kilikuwa ni taka taka tu kwao.
Hawa watu waliandika chochote kuhusu mimi na
watu walinunua magazeti yao.
“honey ,
umependeza kwenye hili gazeti.”
Aliongea mke
wangu akionyesha picha iliyokuwa kwenye moja kati ya magazeti yaliyokuwa
mezani. Ilikuwani picha tuliyokuwa wote
wawili tikiwa tumekumbatiana.
“mbona hata
wewe umependeza malaika wangu.”
Nilimuitikia
.
“No honey
yako ndio nzuri zaidi.”
Aliongea
Judy kwa kudeka.
“okey sawa
sitaki kukuuudhi malaika wangu, nimekubali mimi ndio nimependeza zaidi.”
Niliongea
kwa kumbembeleza.
***
Nae
alisogeza kichwa chake na kuniegamia nikawa na kikuna kuna kichwa chake ,
“nimekudanganya.”
Niliongea .
“nini ?”
Aliuliza kwa
mshtuko.
“wewe ndio
umependeza kuliko mimi.”
Niliongea na
kisha nikicheka , alichukua mto uliokuwa kwenye sofa na kuanza kunipiga nao .
Niliiinuka
kwenye sofa hiyo huku nikikimbia ,
alinikimbiza huku akicheka , tulikimbizana
huku yeye akiwa ameushika ule mto ili anipige nao tena pindi
atakaponikamata.
“oh , oh.”
Nilalamika
pale aliponikamata. Shati langu
“I will kill
you! I will kili you!”
[ nitakuua
nitakuuua.]
Aliongea
huku akinipiga piga na mto.
“sawa mpenzi
nimekoma , nimekoma sirudii tena .”
Nilijaribu
kujitetea lakini yeye aliendelea kunipiga na mto huo .
Nikaudaka na kufanya ashindwe kunipiga nao tena
alijaribu kuuvuta toka kwangu lakini alishindwa sababu nilikuwa na nguvu
kumzidi.
Aliuachia
mto huo kinyonge na kisha kuondoka hapo akikimbia, macho yake yalikuwa
yamelengwa na machozi , muda wowote angeweza kukudondosha machozi.
“honey, am
sorry, honey please wait for me.”
Niliongea
huku nikimkimbilia, haraka haraka alikuwa akipanda ngazi sikuweza kubahatika
kumdaka popote mpaka anamaliza ngazi hizo mimi bado nilikuwa sijamfikia .
Aliingia
chumbani na kwenda kujitupa kitandani .
Na kisha
kuanza kulia kwa kwa kwi kwi.
“mpenzi
tafadhari , usinikasirikie, nakupenda.”
Niliongea
kwa sauti ya upole , wakati huo nilikuwa naogopa hata kumgusa, chochote
nilichokifanya kilichomfanya hadi adondoshe machozi kwa wakati huo kilikuwa kikinihuzunisha
na mimi , kwa kweli sikutamani kabisa kuyaona machozi kwenye uso wa mpezni wangu, yeye ni malaika , hastaili kulia ,
kitu pekee nilichotamani kukiona kwenye uso wake ni tabasamu pamoja na zile
dimpo zinazoonekana kwenye mashavu yake pale anapotabasamu.
Lakini sio
machozi , oh hapana.
“honey ,
sikunuwia kukutoa machozi , tafadhari
naomba unielewe nakupenda .”
Niliongea
huku nikisogea pale kitandani taratibu, nilinyoonya mjkono wangu taratibu ili
angalau niiguse ngozi yake , sikujua ni njia gani ambayo ingeweza kumfanya
atulie, lakini mikono yangu ikishika angalau mabega yake nilitumaini pengine hilo linaweza kumfanya
ajisikie vizuri.
“sikuhitaji
Deo , nenda zako, kaa mbali na mimi.”
Aliongea
huku akiendelea kulia akiwa amejilaza kifudi fudi.
Kusema kweli
kauli hiyo iliniumiza hata zaidi , nilikuwa makini sana na vitendo vyangu
sikutaka kufanya lolote ambalo lingemfanya akasirike hivyo lakini ili jambo
nililolifanya nikiwa na nuwia kumfurahisha zaidi limegeuka kuwa jambo la
kumhuzunisha. Na sasa kitu pekee nacho kitaka kutoka kwangu si faraja , bali
nikae mbali nae.
Sikuwa na
kipingamizi niliinuka kwenye kitanda hicho kinyonge na kuanza kupiga hatua ,
nilipiga hatua ya kwanza ya pili ya tatu nikashtukia ghafla nakumbatiwa kwa
nyuma , alikuwa ni yeye , nilihisi joto lake, ngozi yake laini vyote kwa pamoja
vilileta furaha ya ghafla moyoni mwangu.
“usithubutu
kunyanyua mguu huo na kupiga hatua nyingine , Deo, sababu ukifanya hivyo, naapa
nitakuua.”
Aliongea
Judy kwa sauti yake laini ambayo kila wakati nikiisikia katika ngoma za masikio
yangu nilikuwa nikisisimka kwa hisia , ilikuwa kama melodi nzuri ambazo muda
wote zinaupa faraja moyo wangu.
Alinigeuza
nyuma na nikageuka kumuangalia , ni kweli macho yake yalibadilika rangi sababu
machozi yaliyokuwa yanamtoka , lakini uso wake jinsi ulivyokuwa na tabasamu
pamoja na zile dimpo kwenye mashavu yake , zilinifanya nijisikie kwamba mimi
ndio mwanaume mwenye bahati zaidi duniani.
Kwa sababu
mashavu haya hayakuwa mazuri kwa kuyaangalia tu , bali pia kuyashika na
kuyabusu.
“kamwe
siwezi kukuruhusu ukae mbali na mimi deo.”
Aliongea
maneno hayo kwa hisia huku akiniangalia usoni , naweza kukwambia bwana , macho
yangu hayakupepesa kuangalia mahali popote pale zaidi ya kuyaangalia macho yake
, kwa sababu pale nilipoyaangalia macho yake nilijiona mimi nikiwa ndani ya
macho yake na hicho ndicho kitu kizuri zaidi nilichpenda kukiona katika maisha
yangu.
“hata mimi
siwezi kukuruhusu uniache mwanadani wangu.”
Nami pia
niliongea kwa hisia , kumbatio la sasa lilikuwa ni la nguvu zaidi kila mtu
alikuwa akilihisi. Na vile mikono yetu ilivyokuwa ikipapasa maungo yetu basi
kila kitu kikabadilika kwa wakati huo na kuwa kitu kingine kabisa , midomo yetu
ilikuwa karibu na ndimi zetu ziligusana , na halafu hakukuwa na nafasi ya sisi
kusimama tena , tuliikuta miili yetu ikiwa juu ya kitanda , mito ilidondoka
chini na hata mashuka yalitanduliwa ,
ulikuwa ni mgalo galo tu juu ya kitanda hicho mara tuwe kwenye kona hii ya
kitanda mara ile ,sijui miguu ikishuka
chini ya kitanda kichwa kikining’inia , yani lolote lilifanyika ili mradi
tujisikie burudani zaidi.
***
Juma tatu
siku ya kwanza kuanza kazi tangu nilipo niliporejea nchini , nilipoingia
ofisini kitu cha kwanza kufanya ilikuwa ni kuweka picha yetu ya harusi mezani
kwangu.
Na kisha
nikaitisha kikao cha idara zote ili nijue kilichokuwa kinaendelea ofisini wakati wote nilipokuwa kwenye fungate langu.
“mikataba
miwili imeingia bosi kampuni ya Bikok toka johnseburg, Afrika kusini. pamoja na
Khc kutoka Nairobi Kenya.”
“mliwaeleza
kuhusu harusi.”
“ndio na
wakasema watavumilia, Bikok imekutumia na zawadi pia, lile bmw lililotambulisha
na Bw.Maziku unalikumbuka ?”
“ah sio
rahisi , bmw zilikuwa ngapi unafikiri ? nachokumbuka ni Ndege niliyopewa na
mama yangu.”
Niliongea
kwa madaha , walicheka kidogo kisha kikao chetu kiliendelea.
“na pia
mizigo yote tuliyoitegemea imeingia bila matatizo.”
“kazi nzuri
sana.”
Niliwapongeza
, na huo ndio ulikuwa utamaduni wangu tangu nilipoingia rasmi katika ofisi hiyo
ambayo mama yangu aliianzisha miezi mitatu baada ya kuzaliwa kwangu , huwezi
kuamini nikikuambia hili, nilianza kutia sahihi za ofisi hiyo hata kabla
sijaanza kulitaja jina langu , dole gumba langu lilikuwa likitumika kuingiza
mamilioni wakati mimi hata pesa sijui ni kitu gani na wala kina maana gani
katika maisha na nilipoingia shule masomo yote niliyokuwa nasoma yalikuwa
yakiniongoza kuiongoza kampuni hiyo , na kulikuwa na somo maalumu ambalo
nilikuwa nikifundishwa kujifunza kuhusu kampuni hiyo , ilipo shuka ilipopanda
yote nilikuwa nikipewa taarifa , uzembe uliofanyika na bidii ambayo wafanya
kazi wa kampuni hiyo wameifanya.
Nakumbuka
mtu wa kwanza kufukuzwa kazi kwa amri yangu ilikuwa kipindi nikiwa darasa la
sita.
Nilipewa
lipoti ya mtu aliyeikosesha kampuni tenda ya mamilioni ya shilingi , kwa sababu
alitapika kwenye kikao cha kushindania tenda hiyo na matapishi yake yakawa
yananukia pombe. Na hivyo akaiangusha kampuni ikaonekana inaendeshwa na
wafanyakazi walevi.
Kwa wakati
huo mama yangu aliniambia kwamba , ‘umefanya kitu sahihi’
Na jambo
hilo nilikuwa nalo kwa kweli katika ofisi yangu kila mfanya kazi alikuwa
nalifahamu jambo hilo vema , tulicheka pamoja na kutaniana , lakini ilipofika
suala la uzembe katika kazi , nilikuwa mtu mwingine.
“hii ni
kazi, siko tayari kuona mtu analeta mzaha hapa, Mr John , utawajibika katika
hili , nataka maelezo ya kutosha kuhusu fedha hizo la sivyo utazilipa au
utaozea jela.”
Hivyo ndivyo
nilivyokuwa sikuwa tayari kuona kampuni hii ikiteteleka hata kidogo sababu ya
uzembe wa mtu mmoja.
Sababu
niliamini kwamba kampuni hii imeshikilia maisha ya watu wengi, nilikuwa na
vituo viwili vya watoto yatima waliokuwa wakipewa matunzo yote pamoja na elimu
kwa kutegemea kampuni hii , sikutaka kuwaaangusha watoto hawa na wala sikutaka
kuiaibisha familia yangu kwa kunifunza jinsi ya kuendesha kampuni tangu
nilipokuwa mdogo alafu leo hii kampuni iishie kufirisika, hapana hilo kamwe sikuwa tayari kulishuhudia
likitokea katika maisha yangu.
Baada ya
kikao nilimuita mwana sheria wangu kwa sababu nilitaka kurekebisha mambo fulani
katika kampuni.
Nikiwa
nimeketi na mwanasheria huyo ghafla simu
yangu ya mkononi iliita nilipoiangalia kioo nikaiona picha ya mke wangu , nilitabasamu na kisha kuipokea.
“honey njoo
nyumbani , ninaumwa , njoo haraka please nakufa!”
Mke wangu
aliongea kwenye simu huku akilia na kisha akakata simu.
“hallo! Halo! Halo!”
Niliita japo
kuwa simu ilikuwa imekatika , nilijaribu kuipiga tena lakini haikupokelewa.
Kusema kweli
jambo hilo lilinishtua kupita kiasi, nilishtuka huku akili yangu ikiwa kama
vile imepagawa sikujua nifanye nini au nilekee wapi , kuisikia sauti ya mke
wangu ikisikika kama ambavyo ilisikika muda huo kwenye simu ilikuwa ni mara
yangu ya kwanza .
Nilianza
kuhofia kumpoteza siku hiyo.
“hatuwezi
kufanya hili , nimepata dharula .”
Nilimwambia
mwanasheria huku nikitoka ofisini haraka.
“lakini
bosi….”
Alitaka
kuongea lakini alijua kwamba ameshachelewa kwa wakati huo nisingeweza
kumsikiliza mtu yoyote akisema jambo lolote , hata sekritali sikumuaga nilitoka
mbio huku nikiwa sijielewi kabisa , kichwani mwangu kulikuwa na picha ya mke
wangu akilia na kulalamika , sikujua ni nini kina muumiza , lakini nilijua ya
kwamba natakiwa kuwa pale nikimsaidia kwa lolote.
Sikuwa
tayari kumruhusu afe kwa urahisi namna hii wakati bado namuhitaji.
bado
nilitaka kufurahi pamoja na yeye
Niliingia
kwenye gari haraka , na dereva alifanya hivyo , kisha nikamuamrisha.
“endesha
gari kwa kasi nataka kufika nyumbani sasa hivi mke wangu anatatizo.”
“sawa bosi
.”
Aliitikia na
kisha kuzipangua gia za gari hilo , na kweli kasi yake ilikuwa balaa , japo
kwangu niliona bado kabisa , nilitaka kufika nyumbani kama vile muujiza ili nimuone mke wangu dakika hiyo hiyo.
***
Nusu saa
baadae tuliwasili katika makazi yangu, mimi nilishuka hata kabla gari
haijasimama vizuri na kuanza kukimbia kuelekea ndani haraka.
“judy ! ,
Juddy ! , uko wapi malaika wangu?”
Nilianza
kuita huku nikipanda ngazi za kulekea chumbani kwetu haraka .
Nilipofika
chumbani nikamkuta amelala kifudi fudi huku akiwa amejikunja kwenye kona ya
kitanda .
Kwa
kumuangalia tu nilijua kwamba mke wangu yupo katika maumivu makali , japo
sikujua kinachomuuma.
“mke wangu ,
umepatwa na nini malaika wangu?”
Niliongea
kwa sauti ya upole huku nikitembea
haraka kusogea pala kitandani na nilipofika nilipanda hata bila ya kuvua viatu.
Nilimshika
mabega na kujaribu kumgeuzi ili niweze kuiona sura yake , nilijua ya kwamba
itakuwa imejaa machozi na huzuni tele lakini nilitaka kuiona hivyo hivyo hata
kama matokeo ya kuiangalia yatakuwa ni
kuniliza na mimi pia.
Nilitaka
kuiona ili nimuulize kile kilichomsibu wakati nayaangalia macho yake .
“tafadhari
mke wangu naomba unitazame.”
Niliongea
kwa sauti ya upole na yenye kubembeleza machozi tayari yalikuwa yameshaanza
kuyalenga macho yangu na kile nilichokitarajia sekunde chache zijazo ilikuwa ni
macho hayo kuanza kudondosha machozi.
Nilimgeuza
na pale alipogeuka nilijikuta nashangaa , macho yangu yalidondosha matone ya
machozi yaliyodondoka toka kwenye jicho langu na kwenda kutua moja kwa moja
kwenye mashavu yake , lakini hajabu chozi hilo lililodondoka toka kwenye macho
yangu ndio lilikuwa chozi pekee lililoyagusa mashavu yake kwa wakati huo.
Macho yake
yalikuwa makavu na wala hayakuwa na dalili za kuwa yalitoa machozi hata dakika
kadhaa zilizopita.
Macho yetu
yaligongana kwa sekunde kadhaa huku mimi bado nikishangaa, na kilichofuata baada
ya hapo toka kwa Juddy kilikuwa ni kicheko, alikuwa akinicheka mimi, alinicheka
kwa kuwa alifanikiwa kunifanya mjinga asubuhi hiyo.
Kusema kweli
nilipenda utani lakini huu alioufanya
mke wangu leo hata sikuufurahia , nilifanya kila kitu kwa haraka nikiwa
ofisini nilimshinikiza dereva kwenda mwendo kasi usiokuwa wa kawaida jambo
ambalo lingeweza hata kunifanya nipate ajali na mbali na yote roho yangu
ilikuwa juu juu wakati wote nikimuhofia
lakini matokeo ya yote hayo ni huu utani wake.
“kwa nini
umeamua kunistua hivi malaika wangu jamani?”
Nilimuuliza
kwa upole , japo moyoni nilitamani hata kufoka.
Lakini jibu
nililo lipata toka kwake ni kuchekwa alinicheka kicheko cha sauti ya juu na
kunifanya nizidi kukasirika , lakini kwake ilikuwa marufuku kumuonyesha hasira
zangu, hata niwe nimepita kikomo cha hasira nilitakiwa kuigiza ili nihakikishe
anabaki katika hali ile ile ya kuwa na furaha, najua unaweza kusema mimi nina
wazimu , najua kuna wakati katika maisha yangu niligundua kwamba hata nijighulishe
kwa kiasi gani kamwe sitoweza kuifanya nafsi yangu ikafurahi kwa asilimia zote
, lakini kitu nachoweza kufanya ni kumfanya mtu anifurahie mimi wakati wote na
nilimchagua yeye , ni yeye ndiye mtu pekee ambaye kwa gharama yoyote
nitahakikisha anafurahia kuwa na mimi katika maisha yake yote.
“usifanye
mzaha mke wangu , namna hii unaweza kuniua.”
Nilizidi
kumbembeleza japokuwa kwake bado kilikwa kichekesho alitaka kucheka zaidi ya
hapo .
“nimekupata
leo.”
Aliongea na kuendelea kucheka , hapo sasa
sikuwa na jinsi ili niweze kuendana nae ilinibidi na mimi nicheke pia ,
nilicheka utafikiri kweli nillifurahishwa na hali hiyo .
“jamani
mpenzi wangu usinikasirikie , nilikumisi ndio maana niliamua kufanya hivyo.”
Aliongea mke
wangu huku akiniangalia usoni, kusema kweli pamoja nakuificha hasira yangu
kiasi hicho lakini juddy alikuwa na kipaji cha kuifichua hasira yangu popote
pale ilipo.
Maneno yake
na sauti yake vyote vilikuwa na nguvu iliyokuwa inaweza kuifutilia mbali hasira
hiyo ndani ya moyo wangu.
“sawa mke wangu
, siku nyingine naomba usifanye hivyo , unaweza kuwa na tatizo kweli harafu
mimi nikapuuzia na kufikiri ni moja kati ya huo utani wako.”
Niliongea
kwa upole.
“basi mpenzi
wangu nisamehe , sirudii tena kufanya hivi nakuahidi.”
Aliongea kwa sauti nyororo sauti ambayo
ilinifanya nitulie kimya na kuyaangalia macho yake kwa hisia , sura yake na
uzuri wote alionao vyote vilinifanya nipagawe kwa wakati huo , hakukuwa na
huzuni wala masononeko katika moyo wangu tena bali penzi zito lililojaa uchu.
Nilichokuwa natamani kwa wakati huo ni kuibusu midomo yake , kuishika sura yake
nihisi ulaini wa ngozi yake .
MWISHO WA
KITABU CHA KWANZA , AHSANTE KWA KUFUATILIA SIMULIZI ZANGU,
No comments:
Post a Comment