GIFT KIPAPA

Saturday, July 9, 2016

NOT YOU NOW BOOK 01






NOT YOU NOW BOOK 1
{si wewe kwa sasa}

                 BY D.G.LWASYE 'GIFT KIPAPA'
STORI KWA UFUPI:
Ni stori inayohusu wanafunzi wawili Joel na Grace, hawa walikuwa wanafunzi waliofanikiwa sana katika taaluma tangu waliposhiriki mashindano ya kujieleza kwa lugha ya kiingereza katika mdaharo na kuiletea heshima shule yao, waliishia kuwa wapenzi walioshibana lakini mapenzi yao yanageuka shubiri pale mmoja wapo alipomaliza shule na kumuacha mwenzie akiendelea, hilo bado alikuwa jambo lilililo muumiza yoyote kati yao kiasi cha kutosha kama ambavyo aliumia Grace pale Joel anapomweleza kwamba yeye sio anaye mpenda kwa sasa bali kuna mtu mwingine. Simulizi hii iliyojaa maumivu ya moyo na kutaabika kwa nafsi katika kupigania kulipata penzi tena itakusisimua moyo wako kuliko hata unavyoweza kuvutia picha.

MWANZO:

             USHINDI WA UPENDELEO:     

Kelele za wanafunzi wa sekondari ya Tukuyu iliyopo wilayani Rungwe mkonani mbeya, zilisikika wakiwa ndani ya bwalo la shule yao.
Walikuwa hawasiklilizani kabisa kila mmoja aliongea anachokijua.
Nusu saa iliyopita ndani ya bwalo hilo kulikuwa na mashindano ya kumtafuta mwanafunzi mwenye uwezo wa kujieleza katika mdahalo wa lugha ya kiingereza yani Debate.
Mashindano hayo ambayo hatima yake ilikuwa  ni  kuwapata washindi wawili , wa kike na wakiume ambao watakwenda kuiwakilisha shule yao katika mashindano ya wilaya, wakishinda hapo waingie katika mashindano ya mkoa na baadae mashindano ya kitaifa.
Ushindani huo uliokuwa ukifanyika katika sekondari ya Tukuyu ulikuwa ukifanyika nchi nzima. Na baadae wangetafuta mkali wa kujieleza kwa lugha ya kiingereza kwa taifa zima.
Waliofikia fainali ya mashindano hayo katika sekondari ya tukuyu kwa upande wa wavulana ni .Joel John wa kidato cha tatu na Emanuel mwambuluma wa kidato cha nne. Na upande wa wasichana ni fatuma abdala  wa kidato cha nne na Grace Samson wa kidato cha kwanza.
Muda wa kuwatangaza washindi ulifika na mwakilishi wa majaji alisimama na kuanza kutangaza.
“mshindi wetu kwa upande wa wanaume ni Joel  John.”
Alitangaza jaji huyo , wanafunzi wote walishangilia na kupiga vifijo, makofi na ndelemo.
Kwani hakuna mwanafunzi ambaye alikuwa ajui uwezo wa joel John katika kujieleza kwa lugha ya kiingereza
“haya jamani tulieni tumtangaze mshindi wetu wa kike.”
Aliongea jaji huyo, na kisha wanafunzi wote wlitulia na kutega sikio , kwani kila mtu alikuwa na hamu ya kumjua mshindi huyo.
Wengine walisikika wakinong’onezana na kulitaja jina la Grace kwani wengi walishamtabili Grace Samson kuwa ndiye mshindi, kwani pamoja na kuwa kidato cha kwanza Grace Samson alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuongea lugha ya kiingereza, aliweza kuyapangilia mawazo yake vizuri kiasi kwamba kila alipokuwa akiongea katika mashindano hayo watu walikuwa wakimshangila sana na kumpigia makofi. Alikuwa ni mwanafunzi wa pekee katika shule hiyo kwani haikuwahi kutokea mwanafunzi wa kidato cha kwanza akawa na uwezo wa kujieleza na kuzungumza lugha ya kiingereza kiasi hicho.
“Jamani mshindi wetu ni…”
Kabla hata jaji huyo hajaongea watu walidakia na kuongea kwa sauti.
“GRACE SAMSON.”
“Jamani mimi ndio ninaye tangaza naomba mtulie .”
Jaji huyo aliongea na kisha watu wote wakatulia  ili kumsikiliza.
“mshindi wetu ni  Fatuma abdalla.”
Aliongea jaji huyo na kisha kushuka kwenye jukwaa hilo haraka haraka. Hata mwenyewe alijua amekosea  na ndio maana alishuka haraka. Hakuwa na jinsi hivyo ndivyo ilivyoamliwa pamoja na majaji wenzake.
“aaah, haiwezekani hiyo.”
Wanafunzi walisikika wakipiga makelele kuonyesha wazi kabisa kwamba wamepingana na matokeo hayo.
Majaji wote walikwishaondoka ndani ya bwalo hilo kupitia mlango wa nyuma na kuwaacha wanafunzi wenzao wakipigizana makelele hayo.
Wanafunzi hao waliendelea kupiga makelele hayo huku kila mmoja akizungumza maneno ya kwake
“haiwezekani lazima tufanye mgomo alisikika mwanafunzi mmoja akiongea kwa sauti.
“Ndio hapatoshi leo!”
Wenzake waliitikia kwa sauti kubwa. Waliendelea na makelele huku kila mmoja akidai Grace  ndio anayetakiwa kuwa mshindi.
‘NGLII, NGLIII, NGLIII’
Ilisikika sauti ya kengele. Wanafunzi wote walishangilia uliposikika mlio huo, ilikuwa ni saaa nane na dakika kumi na tano.
Huo ndio muda ambao wanafunzi wa shule hiyo wanakula chaskula.
Maongezi yalibadilika na kuwa katika makundi makundi huku wakitawanyika kuelekea bwenini kwenda kuchukua vyombo vyao vya kulia chakula.
Waliporudi toka huko maongezi yalikuwa mengine kabisa .
Hakuna aliyezungumzia juu ya mdahalo bali ni chakula.
Wengine walilalamika na kuwakaripia wapishi kwa kuwapakulia chakula kidogo , huku wale wasiokuwa na pesa ya kununulia matunda wakiomba omba kwa wenzao walionunua.
Na hata baada ya chakula hakuna aliyelifufua suala la mdahalo bali ilikuwa juu ya mechi kali ya kabumbu ambayo ilitakiwa kucheza kati ya kidato cha pili na kidato cha nne.
Kila mtu al;ikuwa akimsifia mchezaji wake na huku kila mtu akitabili ushindi kwa timu aliyoipenda.
Walipokwenda uwanjani huko ndio ilikuwa balaaa, shamla shamla za mpira zilikuwa zimeshamili kweli kweli. Kuna baadhi ya wanafunzi walikuwa wakizunguka uwanja mzima wakiimba nyimbo za kuitukuza timu yao huku wakitupa vijembe na maneno ya kebehi kwa timu pinzani.
Wengine walipiga ngoma na kucheza wanawake wal;ikuwa wakichweza na wengine walijifunua nguo kabisa kuwa onyeshea utupu timu pinzani, japo hao walinukuliwa majina yao na kilanja wa nidhamu na waliporudi shule walikutana adhabu zao.
***
Grace aliumizwa sana na kitendo cha kutotendewa haki na majaji, moyoni mwake alijisikia kunjwa moyo kupita kiasi, alikuwa amekwishajiwekea asilimia zote mia kwa mia kwamba yeye ndio mshindi wakike katika shindano hilo. Alikuwa akijiamini kwa kuwa uwezo wake ulikuwa wazi kabisa.
Lakini hata hivyo Grace hakutaka kuchukulia suala la kushindwa kama ni tatizo kubwa sana, kwani hata angeshinda lisingekuwa jambo ambalo lingemfanya awe na maendeleo mazuri kwenye masiomo yake, hivyo akaamua kulichukulia suala hilo kama la kawaida tu
Aliamua kusahau kila kitu kuhusu mdahalo na kuweka juhudi zake katika masomo.
Joel John mshindi wa shindano hilo la mdahalo kwa upande wa wanaume alikuwa ni mmoja kati ya watu walioguswa sana na suala la majaji kufanya upendeleao kwa kumchagua fatuma , aliuona uwezo aliokuwa nao fatuma jinsi ulivyokuwa mdogo ukilinganisha na uwezo wa Grace.
Japo grace alikuwa kidato cha chini.
“hii sio haki wala siwezi kukubali.”
Aliwaza joel alipokuwa ameketi peke yake kwenye kivuli chas mojakati ya miti iliyokuwepo  ndani ya shule yao. Alikuwa amepania kweli kuiona haki inatendeka na haki anapata nafasi yake .hakujua kwa nini moyo wake unamsukuma kufanya yote hayo ila alishangaa kujiona ana kiu ya kutaka kuona Grace anatendewa haki.








BARUA YA JOEL            

Alichokifanya Joel ni kuchukua Kalamu  na karatasi kisha akaandika barua ya malalamiko kwa mkuu wa shule, akidai wanafunzi wa kidato cha kwanza hawajatendewa haki katika mashindano hayo japo walikuwa na uwezo mkubwa. Alipomaliza kuandika barua hiyo aliikunja vizuri na kuitia katika bahasha. Usiku muda wakujisomea akaenda mpaka ilipo ofisi ya mkuu wa shule na kuipitisha barua hiyo chini ya mlango..
Kisha akarudi darasani na kuendelea kujisomea kama wanafunzi wengine walivyofanya. Japo yeye alisumbulia wa wanafunzi wenzake waliokuja kwenye dawati yake na kumpa hongera ya ushindi alioupata siku hiyo.
Alishukuru japo moyoni hakuwa na furaha  kwani aliamini ushindi huo usingeweza kukamilika bila ya Grace, alimkubali sana Grace sababu alijua anaweza aliamini kama wangekuwa pamoja katika mashindano hayo basi wangeweza kuiwakilisha vema shule yao katika mashindano hayo.
Ahsubuhi siku inayofuata mida ya saa mbili na nusu wanafunzi wote wakiwa madarasani wakifundishwa na walimu , kengele ililia na kuwashtua wanafunzi wote kwa sababu kengele hiyo haikiuwa ile ambayo ilipaswa kusikika kwa wakati huo ambayo ilikuwa ikiashiria kipindi kuisha , bali kengele hii ilikuwa ile inayoashiria dharula au muda wa masomo kuisha.
Wanafunzi wote walitoka madarasani na kwenda mstalini haraka  ili kujua kile kilicho sababisha kulia kwa kengele hiyo.
Hakuna aliyejua sababu ya kengele hiyo kulia si kilanja mkuu wala mgonga kengele mwenyewe yeye alifuata amri tu aliyopewa na mkuu wa shule.
Ni Joel pekee ndio alikuwa ana hisi hisi tu kwamba huenda ujumbe wake umemfikia mkuu wa shule.
Wanafunzi wote walijipanga kila kidato na mstali wake , walikaa kimya ilikujua kinachoendelea.
Jukwaani alisimama mkuu wa shule na mwalimu wa taaluma, muonekano wa mkuu wa shule uliwatisha wanafunzi wote, uso wake ulikuwa umekunjamana kwa hasira. Jambo hili lilimfanya joel apate uhakika kwamba sasa ujumbe wake umefika.
Kilanja mkuu aliitwa na kukabidhiwa karatasi  awasomee wenzake kilichoandikwa katika karatasi hiyo, alianza kusoma.
“kwako mkuu wa shule , shikamoo, mimi ni mwanafunzi wako naleta malalamiko yangu juu ya jambo alilotendewa mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika mashindano ya kumtafuta mwanafunzi anayeweza kujieleza vizuri katika mdahalo kwa lugha ya kiingereza.
Grace Samson mwanafunzi wa kidato cha kwanza amejieleza vizuri sana na ametoa hoja ambazo kama angepewa nafasi ya kuiwakilisha shule yetu katika mashindano hayo nje ya shule nina hakika angeweza kuleta sifa ambayo kwa hakika shule yetu ingejivunia kuwa naye, lakini kwa kuwa majaji wa shindano hilo walikuwa ni wanafunzi wa kidato cha nne basi wameamua kufanya maamuzi wanavyojua kwa kumpatia mwanafunzi mwenzao wa kidato cha nne aitwaye fatuma Abdalla nafasi hiyo wakati hana uwezo mkubwa kama ilivyo kwa Grace Samson.
 Nimesikitishwa sana na maamuzi haya mkuu, na nina hoji kwamba kuna haja gani ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kuwekwa kwenye mashindano hayo kama watasimama kama vivuli tu? 
Si kawaida kwa shule zetu hizi za serikali ambazo wanafunzi wake wengi wanatokea shule zetu za msingi ambazo zinatumia lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia kuweza kuzungumza na kujieleza vizuri lugha ya kiingereza  kama ambavyo Grace Samson ameweza , bali wengi wanakuwa wakitatizwa na lugha hiyo mpaka kufikia kidato cha pili hadi cha tatu hivi, lakini leo hii mwanafunzi wa kidato cha kwanza ameonyesha uwezo huo na alichoambulia ni kuvunjwa moyo na kupokonywa haki yake.
Ni hayo tu mkuu nimeandika kwako kwa kuwa najua wewe ndio mkuu wa shule hii na ndio mwamuzi wa mwisho katika masuala yote yanayoendelea katika shule hii ili uweze kuliangalia jambo hili na kuhakikisha haki inatendeka, Ahsante.”
Alimaliza kusoma kilanja mkuu.
Wanafunzi wote walishikwa na bumbuwazi huku wote wakiwa wamegeuza vichwa vyao kumuangalia Grace kwani kila mmoja aliamini Grace ndio aliyeandika barua hiyo.
“Ni nani aliyeandika barua hiyo?”
Aliuliza mkuu wa shule , wanafunzi wote walibaki kimya
“narudia tena swali langu , ni nani ameandika barua hiyo?”
Aliuliza tena mkuu wa shule macho ya wanafunzi wote yalikuwa kwa Grace.
“mimi ndio nimeandika.”
Sauti hiyo iliposikika wanafunzi wote waligeuza vichwa vyao kumuangalia mtu aliyeitoa kauli hiyo,  hakuna aliyeamini baada ya kumuona Joel akijitokeza.
“Ni Joel!, jamani mungu wangu!”
ilisikika sauti ya msichana mmoja aliyeongea kwa masikitiko, kwani walichoamini wanafunzi wote ni kwamba Joel amefanya kosa kubwa. Ambalo linaweza kumfanya afukuzwe shule au kupewa adhabu kali. Walifikiria hivyo kwa sababu walimfahamu vyema mkuu wao wa shule, alikuwa hapendi mzaha hata kidogo, alikuwa haoni hasara kumfukuza shule mwanafunzi hata kama akifanya kosa hata kidogo, kesi ikimfikia yeye tu basi hakukuwa na msamaha.
Wapo wanafunzi waliofukuzwa kwa kutovaa tai, soksi na hata kutochomekea shati sembuse yeye ambaye alifikia hatua ya kumuandikia barua kabisa.
Joel aliyajua yote hayo lakini tayari alikuwa ameshaamua kujitoa mhanga, alikuwa tayari hata kufukuzwa shule lakini sio kuiona haki ya Grace inapotea.
Alijitokeza mbele ya jukwaa, wanafunzi wote walikuwa wakimuangalia kwa huruma. Upande wa Grace ndio machozi yalikuwa yakimbubujikka mashavuni , aliumia kuona mtu anataka kufukuzwa shule kwa sababu yake.
Mkuu wa shule alimuangalia Joel na kisha kutoa tabasamu usoni mwake na tabasamu hilo lilikuwa la kwanza tangua aliposimama katika jukwaa hilo ahsubuhi hiyo.
“mpigieni makofi.’
Mkuu wa shule aliamrisha, nukta hiyo hiyo wanafunzi wote walipiga makofi huku wakiwa hawaelewi kwa nini mkuu kawambia wafanye hivyo.
“Vizuri.”
Mkuu wa shule aliongea mara baada ya wanafunzi kumaliza kupiga makofi hayo.
Alikaa kimya kwa nukta kadhaa na kisha kuanza kuongea tena.
“huyu ni mfano wa kuigwa , katika shule yangu hajawahi kutokea mwanafunzi mwenye ujasiri na mpenda haki kama ilivyo kwa kijana huyu.”
Aliongea huku akimuangalia Joel usoni alimpa mkono na Joel aliupokea mkono huo na wakasalimiana kwa mara ya kwanza na mkuu wa shule tangu aanze masomo yake miaka mitatu iliyopita.
“hongera sana kijana kwa ujasili wako.”
Aliogea mkuu wa shule huku bado wakiwa wameshikana mkono.
“ahsante mkuu.”
Aliitikia Joel japo wasi wasi bado ulikuwa haujatoka mwilini mwake.
Mkuu wa shule baada ya kumaliza kupeana mkono na Joel, aliwageukia wanafunzi , ambapo aliwaita majaji wa shindano hilo na kuwakaripia sana , alimgeukia mwalimu wa taaluma naye pia alimkaripia kwa kuacha tukio kubwa  kama hilo lifanywe na wanafunzi wenyewe japo yeye alijitetea kwamba alikuwa na dharula iliyompelekea kutofika kabisa shule siku hiyo.
Hakuishia hapo uongozi wote wa wanafunzi ulikaripiwa mno.  Alimuita Grace mbele akampa pole na kisha akataka pambano hlo lirudiwe muda huo huo na yeye akiwepo, vipindi pamoja na shuguli zote za kiofisi zilisimamishwa kwa muda kisha alitaka wanafunzi wote , walimu pamoja na wafanyakazi wa shule wote wepo katika mpambano huo.
Yani ilikuwa kama baraza la shule ambalo huwa linafanyika mara moja tu  kwa muhula.



MASHINDANO LA HAKI.

Mambo yalionekana hadharani  na kuwafanya ,majaji wa mwanzo waumbuke kwani uwezo wa Grace ulionekana dhahiri, alifanya vizuri kupita kiasi , na kumuacha Fatuma abdalla akijiuma uma na kujikanyaga kanyaga, hadi mkuu wa shule alibaki anashangaa ni utumbo gani huo ulikuwa unaenda kuiwakilisha shule yake katika suala nyeti kama hilo linalo husu taaluma ya shule.
Wakiwa wameboreka na utumbo aliokuwa akiuwasilisha fatuma katika mapambano hayo, Joel aliingilia kati  na kusimama upande wa fatuma na kulifanya pambano hilo libadilike na kuwa ni mashindano ya kujieleza kati ya wavulana na wasichana, hapo kila mwanafunzi alishangilia kwani hoja zilizokuwa zikitolewa hapo kati ya pande zote mbili zilikuwa ni moto wa kuotea mbali, Joel akitoa hoja hii , Grace aliipangua na yeye alitoa ya kwake basi ilikuwa vuta nikuvute kila mwamba ngoma alikuwa akivutia kwake , kilichotokea hapo ni makofi ndelemo na vifijo toka kwa wanafunzi , akiongea Grace wasichana wote walishangilia , akiongea joel wavulana nao walishangilia mjadahalo huo ulikuwa ni wa aina yake katika shule yao kusema kweli hii ilikuwa ni mara ya kwanza kufanyika mdahalo wenye washabiki na uliowakosha wanafunzi kama ulivyokuwa mdahalo huo , yani hadi muda wa kunywa chai uliwapita bila ya wao wenyewe kujua, walikuja kushtuka imefika saa nane mchana ambapo mkuu wa shule aliingilia kati mjadala huo na kusema machache.
“Grace Samson na Joel john, kwakweli sijui nieleze ni jinsi gani ninavyojivuna kuwa na wanafunzi kama nyinyi, katika historia yote ya shule yetu hatujawahi kutuma timu iliyokamilika kiasi ambacho timu yenu imekamilika, nina uhakika nyie mnakwenda kuitangaza shule yetu kuliko ilivyowahi kutangazwa wakati wowote ule.”
Aliongea mkuu wa shule na wanafunzi wote walishangila, hii ilikuwa ni mara ya kwanza wanafunzi kushangilia wakati mkuu wao akiwa kati kati ya maongezi, lakini siku hiyo ilitokea na na hata yeye mwenyewe alijikuta akitabasamu.
Aliongea mengi sana mchana huo na yote yaliwasifia joel pamoja na grace.
Kilichofuata baada ya hapo alimuagiza mwalimu wa taaluma kwamba tangu sasa joel na grace wanatakiwa kuandaliwa muda maalumu wa kufanya mazoezi ya mdahalo , watahilisha masomo yao yote na kuandaliwa timu ya waaalimu ambayo itakuwa inaandaa midahalo mbali mbali yemnye nguvu na iliyowahi kufanyika popote afrika mashariki na walimu hao walitakiwa kuwafua kila siku mpaka siku watakapo enda kupambana na timu  ya shule pinzani, wataandaliwa chakula maalumu na watakuwa  wakipata mafunzo hayo kutwa nzima, wakijadili mijadala mbali mbali katika kila Nyanja ,ziwe za kisiasa , kiuchumi, elimu historian a Nyanja zingine zote.
Kwa kweli jambo hili lilimfurahisha kila mtu katika aliyekuwepo hapo hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa sekondari ya tukuyu kuwekeza nguvu zake katika suala la midahalo, miaka mingine yote suala hilo lilipita kama upepo na wala hawakujaribu kufika katika hatua yoyote .
Lakini leo kwa ushawishi mkubwa wa uwezo waliuonyesha joel na Grace wameweza kumshawishi mkuu wa shule yao kuwa na imani nao.
Ilikuwa ni furaha isiyokuwa na kifani katika shule yao hata majaji waliomnyima nafasi kwa mara ya kwanza walijikuta wakishangilia kama walivyofanya wanafunzi wenzao huku wakizuga zuga na aibu zao zilizokuwa zimewajaa usoni.
Hapo ndipo moyo wa Joel ulipotulia kwani alichokitaka kimekwisha timizika alijisikia amani na furaha tele moyoni kuona Grace amepewa haki yake na pia alijiona sasa kweli anakwenda kwenye mashindano kwani kwa kuwa alikuwa na timu iliyokamilika.
Grace Samson upande wa wasichana na joel john upende wa wavulana kama ilivyokuwa minong’ono ya watu siku za nyuma walipokuwa wakichuana katika mpambano huo kabla majaji feki hawajaaribu mambo.
Grace akutegemea kabisa kwamba angeipata nafasi hiyo. Kichwani kwake alikuwa amekwishafuta kabisa suala la mdahalo na kukubali kushindwa japo haikuwa haki yake.
Lakini leo katika mazingira ambayo hakuyategemea kabisa amejikuta anashindana upya na fatuma na kunyakuwa ushindi wake wa halali.
Alijisikia faraja sana kuona haki yake iliyukuwa imepotea sasa imerejea mikononi mwake, moyoni mwake ilijaa furaha tupu ya kupata nafasi hiyo, hata hivyo hakuona kama furaha yake inaweza kukamilika siku hiyo kama ahatozitoa shukurani zake za dhati kwa Joel , kwani yeye ndio alikuwa ndio chanzo cha ushindi huo ambao yuko kuufurahia.
“lazima nimtafute Joel ili nimshukuru.”
Aliwaza grace akiwa bado yumo ndani ya bwalo ambapo kulikuwa na wanafunzi wenzake lukuki ambao bado walikuwa wakishangilia ushindi ambao ameupata.
Grace aliyapepesa macho yake karibu kila kona ya ukumbi huo na hatimaye kufanikiwa kumuona Joel akiwa na wenzake wakicheka na kufurahi kama walivyofanya wanafunzi wengine katika bwalo hilo.
Grace akaanza kupiga hatua kuelekea pale ambapo joel alikuwa amesimama.
 “Grace !”
mwanafunzi mmoja wa kiume alimuita na kisha Grace aligeuka kumuangalia, alikuwa ni kiche kiche mmoja kati ya wanafunzi wanao sifika sana kwa kucheza kabumbu katika shule hiyo, na ni mwenye rekodi ya kufunga magoli mengi zaidi katika wilaya nzima ya rungwe, japo pia amekuwa na kashfa ya kugombanisha wasichana shuleni hapo kuliko mvulana yoyote Yule.
“Hongera sana.”
Aliongea Kiche kiche huku akitabasamu.
“ahsante .”
Grace aliitikia na kisha kutabasamu pia.
Macho yao yaligongana na wakawa wanatazamana kwa sekunde kadhaa.
“Grace! Grace! Grace! Grace!”
Kiche kiche alianza kuimba huku akipiga makofi , wanafunzi waliokuwepo jirani nae walimuitikia wakaimba wimbo huo wa kumshangilia Grace huku wakimzunguka na kumpigia makofi, wengine walipiga vifijo na ndelemo pia.
Grace alionyesha tabasamu lakini moyoni alikereka kwani kumshangilia kwao kulimfanya achelewe kukutana na Joel kwa wakati huo kama ambavyo alikuwa amepanga , kwani yeye ndio mtu pekee ambaye kama akisema hongera moyo wake ungejisikia furaha ya kweli. Na si hawa wengine wanafiki ambao walibaki kimya siku ya jana wakati haki yake inadhurumiwa.
Dakika tano bnaadae wanafunzi hao walimaliza kumuimbia na hiyo ni kwa sababu walisikia kengele ya muda wa chakula ikilia , kama ilivyokuwa jana walisahau habari yote ya Grace na sasa akili zao zilikuwa zikiwaza chakula tu.
Grace aligeuza macho yake kumuangalia Joel pale alipokuwa amesimama na rafiki zake muda ule wala hakumuona.
Furaha yote aliyokuwa nayo moyoni ilitoweka na huzuni ikatanda ghafla sio siri kuvumilia kukukutana na joel hata kwa dakika moja mbele kulimfanya augue. Hata hivyo hakuwa na jinsi zaidi ya kujipa moyo kwamba atakutana naye wakati mwingine.
“si yupo hapa hapa shule, nitampata tu.”
Aliwaza na kisha kutoka nje ya bwalo hilo na kwenda kuchukua chombo cha kulia chakula kama ambavyo walifanya wanafunzi wengine.
Usiku muda wa kujisomea Grace alipata nafasi ya kumuona Joel, alimkuta akiwa darasani kwao ameketi katikati ya wanfunzi wenzake akiongoza mjadala wa somo la jiografia.
 Grace alisimama pembeni ya wanfunzi hao alishindwa hata kumuita kwa jinsi alivyokuwa ametingwa kutoa maelezo kwa wanafunzi wenzake.
yani kama angethubutu kumuomba joel ainuke hapo basi angeufanya mjadala huo usimame kwa muda. Jambo ambalo kwake aliliona si sawa ilimbidi atoke nje ili asubiri mpaka mjadala huo uishe lakini alipokuwa akipiga hatua za kuondoka Joel alimuona.
“Grace !”
Alimuita, Grace alisimama na kugeuka kumuangalia.
“mbona unaondoka?”
Alimuuliza
“nuimeona jinsi ulivyotingwa na mjadala nafikiri ni vizuri kama nikija baadae.’
“hapana, rafiki zangu wanaweza kusubiri, au sio washkaji?”
“kweli Grace, hata mikiongea saa nzima sisi hatuna noma.”
Aliitikia mmoja kati ya marafiki zake hao na wengine walitikisa vichwa kuonyesha kwamba wamekubaliana na jambo hilo.
“ila hongera sana Grace!”
Aliongea tena mvulana huyo na kisha Grace alimuitikia , wakatoka nje pamoja na joel na kuwaacha rafiki za joel, wakipiga soga zao za hapa na pale.



















PENZI LAIBUKA MOYONI KWA GRACE.

Walienda mpaka kwenye upenu wa darasa hilo , wakasimama hapo na kuanza rasmi maongezi yao.
“Joel nashindwa hata niseme nini au nikupe nini ili nionekane kweli nimekupa shukrani za dhati.”
Aliongea Grace huku akimuangalia Joel kwa macho yake ya kurembua.
“hapana Grace hutakiwi kusema hivyo na wala kuumiza kichwa kiasi hicho, neno ahsante tu linatosha.”
Aliongea Joel kwa kujiamini huku akimuangalia Grace usoni.
“kweli!?”
Grace aliuliza kwa mshangao
“ndio Grace sitaki kabisa uumize kichwa chako kuliwazia suala hili.”
“lakini umefanya kazi kubwa Joel.”
Aliongea Grace kwa sauti yake nyororo.
“najua lakini bado nasisitiza ahsante tu inatosha.”
Aliongea Joel kwa msisitizo.
“okey, thanks a lot Joel.”
[ sawa ahsante sana Joel.]
“your  welcome.”
[ karibu.]
Joel aliitikia kisha wote wawili waliangaliana huku wakitabasamu. Zilipita dakika kadhaa wakiwa katika hali hiyo mpaka mwanafunzi mmoja alipokatiza kwenye upenu huo ndipo walishtuka. Kila mmoja akayapepesa macho yake na kuangalia sehemu nyingine.
“I have to go now, Grace bye.” [ natakiwa kuondoka sasa , kwaheri Grace.]
“okey bye, Joel.” [sawa, kwa heri Joel.]
Grace aliitikia kisha wakashikana mikono ya kuagana ambapo kila mmoja aliondoka kwa kupita njia yake.
Joel alienda darasani kwao na kuendelea na majadiliano na wenzake wakati Grace akishuka chini kwenye madarasa yao.
Alipofika darasani kwao Grace alishindwa kabisa kukaa hata kwa dakika tano kila alipojaribu kufungua ukurasa wa daftari lake ili asome hakuna kilichomuingia, alijaribu kuchukua kitabu cha somo lingine ili aone kama somo hilo litamkubali lakini napo ilikuwa hola , kitabu chake pendwa cha hadithi kiitwacho mine boy kilichoandikwa na mwandishi nguli wa nchini afrika ya kuisini Peter Abraham nacho kilimgomea siku hiyo, aliamua kufunga madaftari yake na kwenda bwenini  huko alijitupa kitandani na kulala chali akiangalia chaga za kitanda cha juu yake.
Mawazo yake yote yalikuwa ni juu ya Joel, mvulana aliyemfanya apate ushindi katika mashindano ya kumtafuta mwanafunzi anayeweza kujieleza vizuri kwa kutumia lugha ya kiingereza katika mdahalo.
Kwani bila jitihada za joel, tayari alikwisha tangazwa ameshindwa.
Japo sifa hizo za joel sio jambo ambalo lilimfanya awe na mawazo juu yake kwa wakati huo, bali ni kitu kingine kabisa nacho ni mapenzi. Kuangaika kote kule darasanai mpaka kushindwa kusoma na kuja kujitupa hapa kitandani huku akigala gala huku na kule katika kitanda hicho ilikuwa ni juu ya mapenzi, Grace aligundua kwamba anampenda Joel.
“I love him, I real do.”
[ninampenda yeye, kweli ninampenda. ]
Aliwaza Grace huku akiendelea kujigalagaza kitandani.
Jambo hili lili muumiza kichwa kweli kweli kwani pamoja na uzuri alionao lakini alijiona si kitu bila ya kuwa na Joel. Ugumu ulikuwa ni jinsi ya kumshawishi Joel kuhusu suala la mapenzi, kwa jinsi alivyoongea nae muda mchache uliopita hakuonekana ni mtu anayefikiria chochote kuhusu mapenzi.
“sijui nitafanya nini Mungu wangu.”
Aliwaza  Grace na kujiuliza maswali ambayo hakupata majibu yake.
Mapema siku iliyofuata Joel na Grace walifuatwa madarasani na kupelekwa katika chumba maalumu ambacho huwa kinatumika kufanyia mikutano mbali mbali ya waalimu.
Huko waliwakuta walimu watano wakiwa wamejipanga na maandalio yao. Kazi ya kujichua kwaajili ya mdahalo ilianza vilitolewa vichwa vya maada mbalimbali na wakaanza kuijadili moja baada ya nyingine  huku kila mmoja akitoa hoja kulingana na upande aliopangiwa uwe ni upande wa kupinga hoja au upande wa kuikubali, wakichuana vikali huku waalimu hao wakiwasaidia pale walipotoka nje ya mstali na pia waliwasaidia namna ya kujenga hoja zilizo na mashiko  walifanya hivyo mpaka ulipofika muda wa mapumziko ambapo chai yao waliletewa humo humo walikunywa na kupewa muda mchache wa kupumzika na kisha shughuli iliendelea ilikuwa ni hoja juu ya hoja walinolewa hivyo kwa muda wa juma zima mpaka muda wa jioni ambao walikuwa wakiutumia kwa ajili ya kujisomea nao pia waliutumia kwa kazi hiyo hiyo.
Waliendelea hivyo hivyo mpaka ilipofika siku ya mpambano wa kumtafuta mwakilishi wa willaya, ambapo shule zote za wilaya ya rungwe zilishiriki na katika mpambano huo walitakiwa kumtafuta mwakili mmoja wa kiume  na mmoja wa kike katika wilaya nzima haijalishi anatokea shule gani. Ili waiwakilishe wilaya yao katika ngazi ya mkoa na baadae ngazi ya taifa kama wakifanikiwa kuvuka ngazi  ya mkoa.
Kama kawaida Joel na grace walitakiwa kuiwakilisha shule yao katika mashindano hayo.
Mpambano ulianza na ulikuwa moto kweli kweli na mwishowe ulifika muda wa kuwatangaza washindi wa mpambano huo ambapo walianza kumtanga za mshindi upande wa wanaume.
“Joel John ndiyo mwakilishi wetu wa wilaya kwa upande wa wanaume.’
Ilisikika sauti hiyo ya jaji ikimtangaza Joel kuwa ndio mshindi , wanafunzi wa shule ya tukuyu sekondari walishangilia kupita kiasi.
Ikafika zamu ya kumtangaza mshindi wa kike.
Wanafunzi wote walitulia na kutega masikio yao kwa makini.
“Grace Samson, kutoka tukuyu sekondari.”
Jaji huyo alimtangaza Grace hapo sasa wanafunzi wa shule ya tukuyu sekondari walikuwa kama vile wendawazimu kwa furaha, waliimba , wariruka na kushangilia  huku wakikimbaia kuelekea shuleni kwao.
Grace na Joel walikuwa wamebebwa juu juu huku wakiimba wimbo uliotaja majina yao na kuwasifia .
Joel alijisikia fahari kubwa kuwa shujaaa wa shule yake, hiyo ilikuwa ni heshima kubwa kwa shule yao tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo shule yao haikuwahi kuwa wawakilishi  wa wilaya.
Lakini leo imewezekana tena kwa kuchukua nafasi zote mbili  ya kike na ya kiume
Jambo ambalo hakuna shule iliyowahi kulifanya hapo kabla, ilikuwa kama mvulana akitokea shule hii basi msichana anatokea shule nyingine. Lakini leo imekuwa kinyume kabisa kwani nafasi zote mbili zimechukuliwa na tukuyu sekondari.






 USHINDI WA MKOA.

Grace nae alikuwa na furaha kupita kiasi alifurahia ushindi mkubwa walioupata nae pia aliamini kwamba hicho ni kitendo cha kishujaa sana kwa shule yake.
Alifurahia kuiwakilisha shule na wilaya yake katika mashindo hayo ya mdahalo wa lugha ya kiingereza .
Lakini furaha yake ilikuwa na dosari moyoni mwake, kwani bado hakuona kama furaha hiyo imekamilika.
Alitamani furaha hiyo ingemkuta akiwa kwenye mapenzi na joel.
Alimpenda sana Joel na alitamani kumuona joel analiona penzi alilonalo kwake ili wawe pamoja katika hali ya kupendana.
“Grace.”
Grace aliisikia sauti hiyo iliyomfanya azinduke toka kwenye mawazo aliyokuwa nayo.
Aligeuza shingo lake kumuangalia mtu aliyemuita.
Hakuweza kuamini pale alipokutana na tabasamu zito la joel,  mapigo yake ya moyo alianza kubadilika na kuanza kwenda kwa kasi, akajikuta ameduwaa na kumuangalia joel.
“hongera Grace.”
Aliongea Joel huku akitabasamu.
Grace kabla ajaongea chochote alimsogelea joel na kumkumbatia.
“hongera na wewe joel.”
“asante .”
Aliitikia.
“lakini yote hii ni kwa sababu yako bila wewe nisingefika hapa.”
“mmmh,mmhh, usiseme hivyo, umefanya juhudi grace , unafikiri ni watu wangapi wamefikia hatua hiyo lakini hawajaweza kushinda.”
“ni kweli joel lakini wewe ndio chanzo cha yote.”
“sawa lakini unajua tumeipa heshima kubwa sana shule yetu.”
“sana.”
“sio sana Grace bado tuna safari ndefu ngazi ya mkoa na taifa zinatusubiri.”
“unafikiri tutafika taifa kweli?”
Grace aliuliza .
“tukisimama hivi wawili , kamwe hatuwezi kuzuilika.”
Aliongea joel kwa kujiamini , kisha wote walicheka.
Walikuwa wakiongea maongezi hayo huku bado wanafunzi wenzao wakiwa shangilia.
Waliporudi shule pamoja na kushangiliwa vile lakini bado walirudi tena kambini kunolewa safari hii walifuliwa mpaka saa tano za usiku, wakiwa na walimu wao watano ambao walikuwa wakiwa pika na kuwa fua ile ile  walitoa hoja na kujibiza na siku nzima huku wakisubiri tarehe ya kwenda mkoani kuchuana na wanafunzi wengine waliokuwa wakiziwakilisha wilaya zao zipatazo nane zinazoujenga mkoa wa mbeya. Japo maandalizi ya nguvu kama ambayo walikuwa wakiyafanya washindani toka sekondari ya tukuyu yalikuwa hayafanywi na shule nyingine yoyote  kwanza hata umoja hawakuwa nao kila mshindani alitoka shule yake na baadhi walitoka katika shule walizokuwa mahasimu hivyo kichwani mwa kila mmoja alikuwa akifikiria jinsi ya kumshinda mwenzake angalau kuchukua namba ya juu kuliko yeye na wengine ile kuwa mmoja kati ya watu kumi na sita  bora toka katika shule zote za mkoa wa mbeya alikuwa sifa tosha kabisa .
Aliona ufahari kukaa katika hoteli kubwa akihudumiwa na serikali kula chochote akipendacho hadi kufikia siku ya pambano.
Muda wa kuwatafuta wanafunzi wawili watakao uwakilisha mkoa wa mbeya katika mashindano ya mdahalo wa lugha ya kiingereza utakao fanyika kitaifa ulitimia.
Wanafunzi kumi na sita kutoka katika shule mbali mbali za mkoa wa mbeya kati yao wakiwemo grace na joel kutoka sekondari ya tukuyu walikuwa tayari kwa ajili ya mapambano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mbeya sekondari.
Mpambano mkali ulifanyika huku kila mmoja akijitahidi kadiri ya uwezo wake kujitutumua kila awezavyo kutema ung’eng’e ili mradi aibuke kidedea katika mashindano hayo na mwisho wa yote washindi wa mashindano hayo walitangazwa
Joel na grace Ndio walioibuka kidedea katika mashindanio hayo, wao ndio waliotakiwa kuuwakilisha mkoa wao katika mashindano hayo ya kitaifa yatakayofanyika katikak jiji la Dar es salaam.
Wakiwa pamoja na mwalimu wao wa taaluma waliruka ruak na kushangilia kwa furaha baada ya kufanikiwa kupata nafasi hiyo ilikuwa ni furaha isiyokuwa na kifani kwao hawakutegemea kabisa kwamba jambo hilo lingewezekana pamoja na kufanya juhudi zote zile, hiyo ilikuwa kama ndoto kwao.
“siamini kabisa Joel.”
Aliongea  grace.
“Hata mimi Grace,”
Joel aliitikia wakiwa wamekumbatiana wakifurahia ushindi wao.
Mwalimu wao wa taaluma alikuwa amesimama pembeni yao nae pia uzalendo ulimshinda akajikuta nae pia ameungana kukumbatiana na wanafunzi wake kwa furaha, sio siri ushindi wa grace na joel ulimfurahisha kupita kiasi , hii itakuwa ni mara yake ya kwanza kupata safari ya kikazi kwenda makao makuu ya elimu tangu aanze kazi.  Tena kwenda makao makuu akiwa mwalimu wa wanafunzi wanaoweza kujieleza vizuri zaidi kwa kutumia lugha ya kiingereza katika mkoa mzima wa mbeya.
Alijua jinsi ambavyo jambo hilo litaipa sifa shule yake na hata yeye pia kama mwalimu wa taaluma.
“mmenifurahisha sana , matumaini yangu mtafanya vivyo hivyo katika mashindano ya kitaifa.”
Aliongea mwalimu kwa furaha.
“bila shaka mwalimu.”
Joel aliitikia.
“kweli kabisa , Mungu yuopo pamoja nasi , lazima tushinde.”
Grace nae pia aliomngea na kisha waliendelea kushangilia ushindi huo huku wakiimba wimbo wa kuisifushule yao,  waalimu pamoja na wanafunizi wa shule hiyo.
Siku hiyo kwao ilikuwa ni furaha kweli kweli .
Wale wanafunzi wa shule zingine walioshindwa wakabaki wakiwashangaa tu.
Moyoni mwa Grace bado kulikuwa na kasoro , furaha yake bado ilikuwa haijakamilika pamoja na ushindi wote huo walioupata , bado akilini mwake alikuwa akifikiria juu ya joel, alimpemnda na alitaka joel alitambue jambo hilo.
Lakini hakuwa na ujasiri wa kumweleza juu ya vile anavyojisikia juu yake.
Aliogopa kumweleza kwamba anampenda sababu alikuwa na wasi wasi kwamba joel anaweza kuwa na hisia tofauti juu ya jambo hilo, kwa kweli suala hilo liliusononesha moyo wake.
“Vip Grace mbona umekuwa kimya hivyo?”
aliuliza Joel mara baada ya kuona Grace amepona kwa muda mrefu.
Swali hilo lilimfanya Grace azinduke toka kwenye mawazo mazito aliyokuwa nayo.
Moyoni mwake aliisikia sauti ikimwambia,
 “mweleze ukweli anaweza kukuelewa, huyo ni mvulana,  wavulana  huwa hawana tabia ya kukataa wasichana wazuri kama wewe.”
“niambie Grace una tatizo gani.”
Joel aliongea kauli ambayo ilikuwa ikimtaka Grace kuongea kile kinachomtatiza kama vile ambavyo mawazo yake yalimtaka afanye .
“ah, hamna tatizo Joel .”
Aliongea Grace haraka haraka  na kujichekesha ili aoneakane kweli hana tatizo.
“sawa nilijua labda una tatizo  kwa sababu nilikuona kimya muda mrefu.”
“hapana joel zaidi  tu nina furaha kutokana na ushindi tulioupata, kama ulivyoseam  joel tukisimama pamoja , hakuna kitakachoweza kutuzuia.”
Aliongea grace kisha wote wawili walitabasamu. Grace hakuwa na maana ya kuwa pamoja katika mashindano ya mdahalo, bali pamoja daima na milele  katika maisha, alitaka kuwa na joel katika kipindi chote cha maisha yake na hakutaka kuzuiwa na chochote kumpata Joel.

















 SAFARI YA DAR ES SALAM

Kilichofuata baada ya joel na Grace kushinda mashindano hayo ya kumtyafuta mwanafunzi anayeweza kujieleza vizuri katika mdahalo wa kiingereza kwa ngazi ya mkoa sasa walitakiwa kusafiri mpaka jijini Dar es salaam, mahali ambapo mashindano ya kumtafuta mshindi wa mashindano hayo kitaifa yalifanyika. Waliingia katika jiji hilo na kufikia katika hoteli ya kifahari iliyokatika ufukwe wa bahari ya hindi  Sea cliff hotel, huko waligharamiwa kila kitu na serikali. Wao ilikuwa ni kufurahia maisha tu.
Ilikuwa ni jambo la furaha sana kwa Joel na Grace kukaa ndani ya hoteli kubwa kiasi hicho ndani kulikuwa na kila kitu , vinywaji vya kila aina, bafuni bafu lilikuwa na maji ya vugu vugu na ya baridi pamoja na jakuzi na mambo mengine kibao ambayo ni ya a hadhi ya nyota tano.
Joel alifurahi kupita kiasi kwa sababu hakuwahi kuota hata siku moja kwamba atakuja kuingia kwenye hoteli ya kifahari kiasi hicho sio yeye tu hata grace pia nae alikuwa na furaha moja ya ajabu mwalimu wao ndio usiseme yeye ndio alikuwa kama chizi muda wote alishinda kwenye jakuzi. Hata habari ya kuwa simamia joel na Grace ili wafanye mazoezi kama ambavyo alikuwa akiwasimamia wakati wapo mkoani kwao hiyo hakuwa nayo, alikuwa akikamua mitungi iliyokuwa kwenye friji mpaka iliimba haleluya.
“unajisikiaje kuwepo hapa, Grace?”
aliuliza joel huku akiwa ametabasamu.
“vizuri sana , natamani maisha yetu yote yangekuwa hapa.”
Aliongea Grace na kisha Joel  akacheka.
“maisha yetu yote!?”
Jole aliuliza.
“Ndio Joel tuishi humu tukiwa tunahudumiwa na wahudumu kama malkia na mfalme .”
Aliongea Grace maneno hayo kwa hisia , kwa sababu alikuwa akiyaongea maneno hayo toka moyoni mwake.
“kwa nini umesema malkia na mfalme?”
Aliuliza Joel huku akimuangalia Joel usoni.
Swali hilo lilimshtua Grace alianza kuwa na wasiwasi kwamba pengine Joel ameshashtukia kwamba yeye anampenda. Japo alipenda jambo hilo litokee lakini alikuwa na hofu nalo kwani hakujua joel angelipokea vipi, mapigo ya moyo wake yalibadilika na kuanza kudunda kwa kasi  sababu ya woga .
“mbona unijibu Grace?”
Aliuliza joel na kumfanya Grace azidi kuwa na wasi wasi, alishindwa kabisa kufungua mdomo na kulitolea maelezo jambo hilo.
“sababu nakupenda.”
Aliwaza Grace kichwani mwake hilo ndilo jibu pekee alilokuwa likimjia kichwani mwake kila alipofikiria kumjibu Joel.  Lakini alikosa ujasiri wa kufungua mdomo wake na kutoa jibu hilo.
Joel hakujua chochote kilichoendelea moyoni  mwa Grace na wala hakuhisi jambo lolote hadi wakati huo.
“Grace!”
Joel aliita baaada ya kimya kirefu kilichokuwepo baada ya joel kushindwa kujibu swali ambalo joel alimuuliza.
“mmh”
Aliitikia grace kwa woga, bado alikuwa na wasi wasi alifikiria bado joel anasubiri jibu kutoka kwake.
“hivi itakuwaje kama tukuishinda?”
aliuliza joel na kumfanya Grace atokwe na hofu aliyokuwea nayo na kurudi katika hali yake ya kawaida.
“nitafurahi joel yani siwezi hata kuelezea jinsi furaha yangu itakavyokuwa.”
Aliongea grace  kwa hisia.
“n a kama ukishinda wewe peke yako?”
Joel aliuliza tena.
“siwezi kufurahi joel , siwezi kufurahi hata kidogo , siwezi kufurahi wakati wewe umeshindwa, nataka tushinde wote Joel  na kama kushidwa basi tushindwe wote.”
“kwa nini?”
“kwa sababu sisi ni wa moja joel , tumetoka mkoa mmoja , wilaya moja , na shule moja.”
“lakini madarasa tofauti.”
Aliongea joel kwa utani  na kisha wote wawili walicheka,.
  “hata kama madarasa mawili tofauti joel lakini mimi na wewe ni wa moja.’
“kivipi?”
Joel aliuliza.
“kumbuka wewe ndio uliyefanya mpaka mimi nikashiriki mashindano haya, unafikiri kama tusinge kuwa wa moja ungeweza kuipigania nafsi yangu kiasi kile , unafikiri ungeweza kujitoa mhanga kwa ajili yangu, unafikiri ungeweza kweli.?”
Grace aliongea maneno hayo kwa hisia huku joel akiwa kimya kumsikiliza kwa makini, Alishindwa kabisa kuongea chochote maneno aliyoongea grace yaliugusa kweli moyo wake,  alijikuta anapoteza tabasamu alilokuwa nalo usoni mwake na kuyafikiria maneno ya Grace , japo hakujua grace alimaanisha nini kuongea maneno hayo.
Akili yake ilirudisha nyuma mawazo na kukumbuka jinsi alivyompigania grace mpaka kufanikisha aingie katika mashindano hayo.
Lilikuwa ni jambo lililohitaji ujasiri wa hali ya juu na hata  kumuingiza katika hatari ya kufukuzwa shule lakini yeye bila kujali kufukuzwa shule wala lolote lile alijikuta anafanya jambo hilo kwa ajaili ya Grace, sio kwa ajili yake bali kwa ajili ya Grace.
“Grace ni nani kwangu?”
aliwaza Joel  na kuwazua lakini hakupata jibu lolote kichwani mwake , kusema kweli hadi wakati huo alikuwa hajui lolote lililomfanya mpaka apigane kiasi hicho kwa ajili ya msichana huo.
“nikisema nilitaka kuona haki ikiitendeka, mbona nimewahi kushuhudia watu wengi wakidhurumiwa haki zao lakini kamwe sikuwahi kuwa hangaikia? Kwa nini nilisimama kwa sababu ya Grace , Grace ni nani kwangu?”
Alizidi kuwaza Joel na mawazo hayo yalizidi kumuumiza kichwa.
“Joel vipi, mbona umekuwa kimya hivyo?”
aliuliza Grace kwa mshangao baada ya kuona Joel amebadilika ghafla.
“Grace nahitaji kuwa peke yangu kwa wakati huu, tafadhari naomba uniruhusu niende chumbani kwangu.”
Aliongea Joel mara baada ya kuona mambo yamemzidia.
Grace alishangazwa na kauli hiyo na wala hakuitegemea.
MWISHO WA KITABU CHA KWANZA


No comments:

Post a Comment